ZAWA WAKUMBUSHWA AHADI WALIOIWEKA KWA WANANCHI GOMBANI NI KUHUSU KUMALIZA TATIZO LA MAJI SAFI NA SALAMA.
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA.
UONGOZI wa Shehia ya Gombani wilaya ya Chake Chake Umeikumbusha Mamlaka ya Maji Zanzibar Zawa Ofisi ya Pemba kuhusu Kukosekana kwa huduma ya Maji Safi na salama katika baadhi ya vijiji jambo ambalo limekuwa likiendelea kuwaathiri siku hadi siku walioahidi kulioatia ufumbuzi Mwanzoni mwa Mwezi wa January 2023.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Sheha wa Shehia ya Gombani wilaya Ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba Subira Khamis Kombo Alisema kuwa Licha ya Ahadi walioekewa kutoka kwa Mamlaka hiyo Kuwa Suala la kukosekana kwa huduma hiyo ya Maji Safi katika baadhi ya vijiji vya Gombani kupatiwa ufumbuzi Mwanzoni mwa Mwezi huu lakini bado hakuna Taarifa zozote juu ya suala hilo.
Alisema Wananchi wake bado Wanaendelea kusumbuka kutokana na kufuata Huduma hiyo Maeneo ya mbali huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake na watoto.
"Tuliambiwa Tuvute Subra Mpka Mwanzoni Mwa Mwezi huu wa Januari 2023 Lakini Naona kimya tu Ndicho Kilichotawala Sijui hata Wananchi wangu niwajibu nini juu Ya Maji ya Zawa Alisema.
Akizungumza Asha Sleiman Mkaazi wa Gombani Alisema kuwa usumbufu huowanaokumbana nao Wakubwa na wadogo Katika baadhi ya Vijiji Shehiani humo unarudisha Nyuma Harakati zao.
Akizungumzia Suala hilo Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mamlka ya Maji Zanzibar Zawa Ofisi ya Pemba , Afisa Mahusiano wa Mamlaka Hiyo kisiwani Humo Sleiman Anass Massoud Aliwataka Wananchi Hao kuendelea kuwa Wastahamilivu kwani Mradi utakaonufaisha Upatikanaji wa Huduma ya Maji vijiji Vya Gombani Umefikia Hatua Nzuri.
"Matarajio Yetu tulikusudia Mwanzoni Mwa Mwezi huu Tatizo la Maji baadhi ya Vijiji Gombani libaki Historia tu Lakini Kutokana na Sababu zilizokuwa Nje ya Uwezo Wetu Mradi huo Utamaliza Mwisho wa Mwezi wa March Mwaka huu 2023.
Anass Alitaja Sababu hizo na Kusema kuwa " Baadhi ya vifaa vyao Vya Ujenzi na ulazaji Mabomba Vilizuiwa Bandarini Unguja Kwa hiyo Mafundi wakachelewa Vilikuwa havitoshi kukamilisha kwa wakati Mradi, Mabomba, Viungo, Pampu, Saruji, Kokoto, Nondo, na Magari ya Kukorogea Zege" Alisema.
Akizungumzia Suala la Utolewaji Taarifa kwa Wananchi juu ya Hatua za Ujenzi wa Mradi huo Sleiman alisema kuwa Mamlaka ilitumia vyombo vya Habari mbali mbali kuwajulisha wananchi.
" Hatukumfata kila Mtu kwake lakini katika Media ZBC Redio Tv, na Radio Jamii na baadhi na Vikao vya Masheha Wilaya zote Tumewambia nini kinaendwlwa kwa sababu Mradi wa Maji Gombani ni moja kati ya miradi inayotekelezwa kwa fedha za ahuweni ya Uviko 19.
Aidha alisema kuwa Mamlaka imelenga kuimarisha Huduma ya Maji kwa kuongeza idadi ya Visima vya Maji vitakavyo Hudumia Chake Chake ikiwemo Gombani.
Shehia ya Gombani yenye wakaazi 4835 ambao wao ni Wanawake na Watoto wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli zao kwa wakati kutokana na usumbufu wa kukosa Maji baadhi ya Maeneo kwa Zaidi ya Miezi Saba Sasa na hulazimika kuyafata Masafa ya mbali huku baadhi ya Maeneo kupata kwa Mgao usiku usiku ambapo Mnamo siku ya Tarehe 16/12 2022 Uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar zawa ofisi ya Pemba walidai kuwa Suluhu ya Usumbufu huo itakamlika Mwanzoni mwa Mwezi huu kutokana na kuendelea kwa ujenzi wa mradi visima pamoja na Ukazaji wa Mabomba yakusambazia Maji.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment