WAJASIRIAMALI KILIMO CHA MBOGA MBOGA WALIA KUKOSA MAJI YA WAIOMBA SERIKALI NA WADAU KUWAANGALIA KWA JICHO LA HURUMA NI KILIMO KINACHOWAINGIZIA KIPATO .
NA YUSSRA SAID - UNGUJA
WANAWAKE wa kikundi cha kijambo chetu Shehia ya Kama ambao wanajishughulisha na ukulima wa mboga mboga na matunda wameeleza kushindwa kufikia kiwango cha uzalishaji wanachokihitaji kutokana na kuaharibika kwa miundo mbinu ya kisima chao cha umwagiliaji.
Wakizungumza na muandishi wa habari hii huko kijijini kwao kama wamesema takriban miezi sita sasa tangu kisima hicho kuharibika hivyo wanakosa maji ya kumwagilia na kupelekea kufuata maji sehemu ya kando ya mashamba yao.
Asha Sadik Abdallah ambae ni mwenyekiti wa kikundi hicho amesema kilimo cha mboga kinawasaidia sana katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwani kwa siku hupata Zaidi ya 10000 hivyo amewaomba viongozi wao kuwasaidia kuwatatulia changamoto hiyo ili waendelee kujipatia kipato.
Nae Msimu Ali Kombo ambae ni mwana kikundi hicho amesema kuanzishwa kwa kikundi hicho cha kina mama kimesaidia kuwahamasisha kujikita na shughuli za kilimo kwani kilimo cha pamoja ni tofauti na kilimo cha mtu peke yake isipokuwa wanarudishwa nyuma na baddhi ya changamoto ikiwemo maji ya kumwagilia.
“Maji ndio kilio chetu kikubwa hatuna maji ya uhakika ya kumwagilia” amesema .
Khamis Ali ni miongini mwa wakulima katika eneo la Kama Amesema wanawake wengi katika eneo la Kama wameamua kijiajiri katika kilimo cha mboga mboga na matunda ambacho kwa kwa kiasi kikubwa kimepunguza kuwa tegemezi kwa waume zao.
Sheha wa Shehia ya Kama amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kwa wakulima hao na am Sheha wa Shehia ya Kama Salim Said Seif amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na amewaomba viongozi wenzake washirikiane katika kulitatua ili wanawake hao waendelee na shughuli zao zao za kimaendeleo.
“Katika shehia yangu wanawake wengi wamejikita katika kilimo lakini kuna changamoto moja inayoturudisha nyuma maji……maji kwakweli yantuumiza vichwa”Amesema
Diwani wa wadi ya Kihinani Ali Haji Haji amesema hana taarifa ya kutokea kwa tatizo la kuharibika kwa kisima cha eneo lao ambacho wanatumia wakulima kwa ajili ya umwagiliaji ,hivyo ameshauri wananchi wanapopata changamoto hasa za kimaendeleo kutoa taarifa kwa viongozi ili waweze kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha ameahidi kulitatua tatizo hilo na kuhakikisha wakulima hao wanafanya shughuli zao hizo ili waendelee kujipatia kipato chao.
Comments
Post a Comment