WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUWASAIDIA KUPATA MELI TANGA PEMBA
Na AMINA AHMED MOH’D- PEMBA.
WANANCHI na Wafanya Biashara wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba wanaochukua bidhaa mbali mbali kutoka Mkoa wa Tanga na kuleta Wilayani Humo Wamemuomba Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DkHussein Ali Mwinyi Kuwasaidia Usafiri wa uhakika ambao utawarahisishia kusafiri wao na bidhaa zao.
Wametoa Ombi hilo Huko katika Bandari ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba walipokuwa wakizungumza na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo iliyifika bandarini hapo kwajili yawafanya wanaosafirisha bidhaa kwa kutumia usafiri wa Baharini unaotambulika kwa jina la Majahazi na kutumia Bandari zisizo rasmi kushusha Mizigo yao ya biashara .
Walisema kutokana na kukosa usafiri wa Uhakika wa kutumia kusafirisha bidhaa zao za Biashara Hulazimika kupanda Majahazi wao Pamoja na Mizigo yao Na kulazimika kushuka Bandari yeyote ambapo hupelekea kuhatarisha Maisha yao wao na Mizigo yao ambayo ndio Tegemeo lao la kuendesha harakati zao Kiuchumi.
Kuna Changamoto zinatupata sisi kama wafanya biashara ambao tunasafiri kufuata bidhaa nje ya kisiwa hichi Tunazifata Tanga, Tunalazimika kutumia Mbadala huu wasafiri na wafanya biashara kwutoka Pemba Tunaiomba Serikali Itutafutie Mbadala ili kusijitokeze mambo ambayo sisi hulazimika kuyafanya kutokana na kukosa mbadala Hamisa Apolinali
Comments
Post a Comment