WANANCHI :VIONGOZI WANAWAKE WANAO UWEZI KUSHIKA NAFASI ZA JUU.
Na Khadija Rashid Nassor Pemba WANANCHI kisiwani Pemba wamesema ipo haja kwa wanawake kujitoa kushiriki katika ngazi za maamuzi ipaswavyo kwani ni wachangiaji wazuri wa maendeleo nchini. Wakiz ungumza na mwaandishi wa habari wakaazi wa wadi ya Michenzani wamesema kuboreka kwa miundombinu ya barabara kijiji cha shangini ambayo imetataliwa na juhudi za diwani mwanamke Mashavu Juma Mbarouk kupitia mfuko wa jimbo imekua chachu kwa mama wajawazito na wazee kufikia huduma ya afya kwa urahisi. Mwanajamii Fatma Mohd amesema kadhia hiyo imedumu kwa miaka kadhaa hali iliyopelekea kwa wanawake wajawazito kujifungua njiani na hata kupoteza maisha ya watoto wao. Kwa upande wao Rehema Omar Salim Ali wamepongeza juhudi za diwani huyo kutakana na hatua anazozichukua kutatua changamoto hiyo ya muda mrefu kwani imewasaidia wanajamiia kufika kwa urahaka katika vituo vya afya. Mashavu Juma Mbarouk Diwani wa wadi ya Michenzani amesema juhudi hiyo imekuja baada ya kuguswa na changamoto hiyo na kusimama kwa ...