WANANCHI :VIONGOZI WANAWAKE WANAO UWEZI KUSHIKA NAFASI ZA JUU.

Na Khadija Rashid Nassor Pemba

WANANCHI kisiwani Pemba wamesema ipo haja kwa wanawake kujitoa kushiriki katika ngazi za maamuzi ipaswavyo kwani ni wachangiaji wazuri wa maendeleo nchini.

Wakizungumza na mwaandishi wa habari wakaazi wa wadi ya Michenzani wamesema kuboreka kwa miundombinu ya barabara kijiji cha shangini ambayo imetataliwa na juhudi za diwani mwanamke Mashavu Juma Mbarouk kupitia mfuko wa jimbo imekua chachu kwa mama wajawazito na wazee kufikia huduma ya afya kwa urahisi.
Mwanajamii Fatma Mohd amesema kadhia hiyo imedumu kwa miaka kadhaa hali iliyopelekea kwa wanawake wajawazito kujifungua njiani na hata kupoteza maisha ya watoto wao.
Kwa upande wao Rehema Omar Salim Ali wamepongeza juhudi za diwani huyo kutakana na hatua anazozichukua kutatua changamoto hiyo ya muda mrefu kwani imewasaidia wanajamiia kufika kwa urahaka katika vituo vya afya.
Mashavu Juma Mbarouk Diwani wa wadi ya Michenzani amesema juhudi hiyo imekuja baada ya kuguswa na changamoto hiyo na kusimama kwa nafasi yake ili kuendana sambamba na dhima halisi ya uongozi na kiongozi bora.

 Kwani kilichomsukuma kuingia katika harakati za uongozi ni kusaidia jamii na kutatua changamoto zinazowakabili wanachi wenzake sambamba Kuonesha uthubutu kwa wanawake wenzake katika kuingia kwenye harakati za uongozi.
Wilaya ya Mkoani ina jumla ya wadi 18 ambazo 9 zinaongozwa na madiwani wanawake na 9 Madiwani Wanaume ni sawa na asilimia hamsini kwa hamsini katika uongozi.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI