WANANCHI PEMBA WAFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA VIONGOZI WANAWAKE.



NA AMINA MASSOUD JABIR. 
Pemba. 

WANAJAMII Wilaya ya Mkoani wamewapongeza madiwani wanawakew wilayani humo kwa umoja wao na utendaji wa kazi zao lengo kuletea maendeleo endelevu.Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema viongozi wanawake ni chachu ya maendeleo kwani wapo mstari wa mbele kutatua changamoto zinazowakabili ndani ya jamii.

Rehema Juma Othman na Maimuna Haroub Sheha, kutoka kijiji cha kizungu shehia ya Michenzani wamesema kupitia jitihada za diwani wa wadi ya michenzani mashavu juma mabrouk zimepunguza tatizo la barabara kutoka michenzani kwenda kijijini kwao jambo linaloashiria maendeleo kupitia kiongozi huyu.
Nao, Salim Kombo na Tabia Makame wanajamii shehia ya kangani wamesema kupitia diwani mwanamke wa Wadi hiyo Mayasa changamoto ya maji imekuwa hostiria kijijini hapoSheha wa Shehia ya Michenzani Juma Nassor amesema juhudi za viongozi hao ni za kupigiwa mfano kwani zimekua hamasa ya kubadilisha mitazamo kwa jamii wanaopiga vita wanawake kushiriki kwenye ngazi za maamuzi.
Mayasa Said Makame Diwani Wadi ya Kangani na Mashavu Juma Mbarouk Diwani Wadi ya Michenzani wamesema hatua hizo zimekuja ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi walizoweka wakati wa kuomba ridhaa samba na utekelezaji wa misingi ya utawala bora.

Utendaji kazi wa viongozi hao zinatiliwa mkazo na kauli ya Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi kwani katika  maadhimisho ya miaka 2 ya Uraisi wake ameweka wazi utendaji kazi wa viongozi wanawake kwa kusema Mawaziri Wanawake wanafanya vizuri ukilinganisha na Wanaume hali inayompa hamsa kuongeza watendaji wa jinsi hii. 
MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI