WANANCHI MKOA WA KASKAZINI PEMBA WAVUTIWA NA MBUNGE MAIDA

Na Khadija Rashid Nassor Pemba

Wananchi Mkoa wa Kaskazini Pemba wamepongewza juhudi zinazochukuliwa na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kaskazini Pemba Maida Hamad Abdalla Katika kuwaletea maendeleo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi Saumu Moh’d Said Diwani wa kuteuliwa Jimbo la Wingwi na  moh’d haji mwanajamii shehiya ya micheweni wamesema, kiongozi huyu amekua akijitoa kwa moyo mmoja katika kusaidia jamii bila kujali itikadi za dini wala siasa jambo limechangia chachu ya maendeleo Mkoani wa Kaskazini Pemba.

Wameongeza kuwa, juudi zake ni nyingi kwani amekua akiwafikia hadi wanajamii wa tabaka la chini kujua changamoto zinazowakabili na kuwapatia suluhisho muafaka na kwa muda hitajika kwani hivi karibuni wamepatiwa vyarahani 14 lengo kubwa wanawake wilaya y micheweni kujikwamua .

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahaya amesema anapata mashirikiano ya kila hatua na kiongozi kutoka kwa bi Maida ili kuwapatia maendeleo wanajamii jambo linalomuongezea hamasa na ari kwenye utendaji wa majukumu yake kwa jamii.

Maida Hamad abdallah Mbunge wa viti maalum mkoa wa Kaskazini Pemba amesema kinachomsukuma kufanya hivyo ni kuona jamii nyingi za tabaka la chini hususan wanawake na wanaoishi vijijini bado hawajafikiwa ipasavyo katika kupatiwa maendeleo.

Ameongeza kuwa ili uwe kiongozi bora ni vyema kusikiliza watu wote bila ya ubaguzi sambamba na kuwaomba wanawake kutumia fursa wanazopatiwa ili kujikomboa kwenye umasikini na kuachana utegemezi kutoka kwa wenza wao ambapo huchangia kwenye masuala ya ukatili na udhalilishaji.

 

 


Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI