MWAKILISHI BAHATI AWEZESHA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE.
- Get link
- X
- Other Apps
Na Amina Massoud Jabir Pemba.
WANAWAKE Jimbo la chambani wamesema juhudi zinazochukuliwa na Mwakilishi wa jimbo hilo za kuwajengea uwezo wa kujiajiari ambapo ni moja ya mambo muhimu yakupigiwa mfano katika harakati za kuleta maendeleo nchini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Hadia Ismail na Nuwaira Karim wamesema elimu ya utengenezaji wa Medera ya batiki imebadilisha maisha yao kwani kwa sasa wameweza kujiajiri.
Wanasema Nuwaira na Karim na Hadia Ismil,
“ jitihada zinazochukuliwa na kiongozi mwanamke Bahati Khamis ya kuwapatia elimu ya ujasiriamali imewatoa mashimoni kwani wamejikomboa na umasikini na hata kuachana na utegemezi kwa wenza wao”.
Kwa upande wake Mwakilishi Bahati Khamis Kombo amesema hatua hiyo imekuja baada ya kuona fursa ya ujasiriamali na jinsi inavyokomboa wanawake na vijana na hatimae kuondokana na utegemezi, pia ni chanzo cha kushiriki kwenye ngazi za maamuzi sambamba na kuchangia kwenye pato la taifa.
“Nikiwa napitia video kwenye mitandao ya kijamii niliiona hii fursa na nikaona sasa nimepata mkombozi wa wanawake na vijana, hivyo nikaanza mikakati ya kubajeti mshahara wangu na hatimae nikamleta huyu Mkufunzi kuwafundisha” Anasema Mwakilishi Bahati.
Sheha wa shehiya ya angwachani Issa Ismail Juma akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema juhudi anazozifanya Mh, Mwakilishi Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo ni za kupigiwa mfano kwani ameonesha kwa vitendo uwezo mkubwa wa uongozi wlionao viongozi wanawake.
Jumla ya vikundi vitano kutoka jimbo la Chambani vimepatiwa elimu ya ujasiriamali na mwakilishi mwanamke wa jimbo hilo lengo likiwa kutatua changamoto ya umasikini.
MWISHO.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment