WANAJAMII MTENG’OMBE,MIAMBONI WAMPATANO MWAKILISHI JIMBO LA CHAMBANI.
Na Khadija Rashid Nassor Pemba
Wanajamii kijiji cha Mtengombe na Miamboni Wilya ya mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, wameshukuru juhudi zinzochukuliwa na Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo katika kuwaletea maendeleo.
Hayo yamezungumzwa na mwanajamii, Kaije Faki na Rajab Said Mohd wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Mteng’ombe wamesema, hawajawahi kufikiwa na huduma ya umeme tangu Mapinduzi ya mwaka 1964 lakini kupitia kiongozi mwnmke Bahati Khamis imekuwa faraja kwao kwani amekua nao bega kwa bega hadi huduma hiyo ilipopatikana.
Bahati Khamis Kombo Mwakilishi Jimbo la Chambani amesema, ameamua kulivalianjuga suala hilo la umeme kutokana na umuhimu wa umeme katika jamii.
Miza Hasan Faki katibu tawala Wilaya ya Mkoani ambae pia ni mwanaharakati Wilayani humo amesema kiongozi Bahati Khamis Kombo amekua na jicho la kuona mbali hivyo ni vyema kwa jamii kuthamini juhudi zake ili kupata maendeleo zaidi.
Sheha wa shehiya ya Ngwachani Issa Ismail Juma, ameshukuru juhudi za kiongozi Bahati kwani amekua akimshirikisha kila hatua ya maendeleo ndani ya shehiya yake na shehiya jirani lengo kupata wigo wa kimaendeleo.
Comments
Post a Comment