Shamra Shamra Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani Yaleta Faraja kwa Wanafunzi 300 Wakike Pemba.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA.
JUMLA Ya wanafunzi Wakike 300 Wa Skuli Za Sekondari Msuka Na Chamabani Kisiwani Pemba Wamepatiwa Elimu Juu ya Mafunzo ya Hedhi Salama, Ukatili wa kijinsia, Pamoja na Haki ya Hedhi salama kwa Mwanafunzi wa Kike, ambapo 233 kati ya Hao wamepatiwa Taulo za Kike Zenye uwezo wa kudumu Miaka Miwili Kutoka ikiwa ni Shamra shamra Za kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Kila ifikapo Tarehe 8 Mwezi wa 3 Duniani Kote.
Elimu pamoja na Msaada wa Taulo hizo kwa Wanafunzi hao umetolewa Na Shirika lisilo la Kiserikali La Smile for Community ikiwa ni katika utekelezaji wa Mradi wake wa Run for Binti Marathon, ambao Umefadhiliwa na Shirika la Msaada wa Kisheria Legal Services Facility unatekelezwa kwa LSF na kyfanya kazi kwa kushirikana na Kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto , Maisha Bora Faundation ZMBF, Taasisi ya Weza, Pamojana Taasisi ya Waja Mama.
Akizungumza na habari hizi mara baada ya kumaliza kutoa Elimu kwa Wanafunzi hao Afisa Mradi kutoka Shirika la Smile For Community Anet Kiao Alisema kuwa lengo la kutoa Elimu juu ya Suala hilo ni kuhakikisha Wanafunzi wakike waliopo Maskulini wanakuwa Salama Wanapokuwa katika Kipindi Cha Hedhi Na kiweza kuendelea vyema na Masomo bila kupata usumbufu na wasi wasi wowote utakaowapelekea kushindwa kufanya vizuri katika Masomo yao na badala yake waweze kuedelea kubaki skuli kuendelea na Masomo yao.
"Lengo la kugawa Taulo hizi kwa wanafunzi wakike ambao wameshafikia umri wa balehe ni kuona wanaondokana na usumbufu wanaokumbana nao wakati wa Hedhi, wanapokuwa Shuleni ambao kwa namna moja ama nyengine hupelekea kukatisha Masomo yao au kushindwa kufanya vizuri Darasani wanapokuwa katika hali hiyo kupitia Elimu hii tuliyoitoa kwa wanafunzi hawa watajua sasa nini wafanye wanapokumbana Na suala hili.
Akitoa Elimu ya Kisheria kwa Wanafunzi hao Alphonce Mbarambe Gura Mwanasheria Kutoka Taasisi ya Legal Service Facility Zanzibar Aliwataka Wanafunzi hao Kutokaa kimya Wanapokumbana changamoto yeyote inayotokana na Hedhi kwa vile Suala hilo linatambulikana kikatiba kama ni haki ya Msingi kati ya Haki za Binaadamu kwa vile Suala hilo linagusa Moja kwa Moja utu wa Wanafunzi hao Wakike.
"Lazima suala la Hedhi Salama liangaliwe kwa Upana wake Hivyo ni lazima Watoto wakike Wenyewe muweze kujua ni jinsi gani suala la hedhi Salama Ni Muhimu kwenu, Mna haki ya kupata vifaa vya kujisitiri kwa gharama nafuu ambavyo ni salama , kupata Mazingira Wezeshi Skuli na Nyumbani ya kubadilishia nguo maji ya Salam vtite hivi Mnahaki ya kudai Endapo mtakuwa Skuli ama Majumbani.
Nao Baadhi ya Wanafunzi waliopatiwa Elimu Juu ya Masuala hayo Akiwemo Fatma Abdalla Mbarouk Kutoka Skuli ya Msuka Sekondari Pamoja Ruwaida Salum Hamad Wamewashukuru Wafadhili hao waliojitolea kuwafikishia Elimu hiyo ambapo wamesema itawasaidia katika kukabiliana na changamoti ambazo walikuwa wanakumbana nazo awali kabla ya kupata Elimu hiyo.
Tunaahidi kuifanyia kazi Elimu hii ili isiwe kikwazo tena kwetu kupata
Changamoto zinazopelekea kuwa watoro tunapokuwa katika Hedhi Alisema Fatma Abdalla Mbarouk.
Tunawaomba na Mashirika Mengine pamoja na Taasisi waoge Mfano huu mzuri ambao utasaidia kufanikisha malengo ya Wanawake tuliyojiwekea Kwani bado Elimu hii na Taulo hizi Wapo wanafunzi wengi ambao wanazihitaji katika skuli nyengine Akaongeza Ruwaida.
Elimu iliyotolewa kwa wanafunzi hao ni Pamoja na na Namna ya kujikinga na kutambua Viashiria vya Ukatili wa kijinsia, Matumizi salama ya Taulo za kike za kufua, Pamoja na Haki ya Kisheria ya Afya ya Hedhi Salama kwa Wanafunzi wa kike Mskulini ikiwa ni shamra shamra za kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ambapo ugawaji wa Taulo hizo Zimepatikana kupitia kupitia Kampeni ya Twende pamoja Run for Binti Marathon.
Mwisho
Comments
Post a Comment