AFYA YATILIWA MKAZO KWA WANAWAKE

NA ASIA MWALIM  UNGUJA. 

KATIBU Mkuu Wizara ya Kazi na Uwezeshaji, masuala ya kazi na Uwezeshaji Zanzibar, Maryam Juma Abdallah, amesema bila ya wanawakwe kuwa na afya nzuri, hawawezi kujenga uchumi imara wa nchi.

Aliyasema hayo wakati akikabidhi taula za kike, nguo za ndani na sabuni kwa wanafunzi 145, kutoka kituo cha kinamama cha umeme wa jua (Barefoot College) na Taasisi ya Dnata, ikiwa ni miongoni mwa harakati za kuadhimisha siku ya wanawakwe duniani, huko skuli ya Matemwe Kijini, Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

Alisema wanawake ni viongozi na walezi wa familia wanapaswa kutunza na kuimarisha afya zao kwa lengo la  kufikia maendeleo yao na taifa kiujumla.


Naibu alisema, Zanzibar kama zilivyo nchi nyengine duniani inasherehekea siku ya wanawakwe, kutokana na umuhimu wake wa kumuwezesha mwanamke kupiga hatua muhimu za kimaisha na kukumbusha jamii juu ya haki za wanawake.

Alieleza kuwa hatua ya kugawa vifaa na kutoa elimu ya afya skulini hapo, ita wawezesha wanafunzi wakike kushiriki vizuri masomo yao bila ya kusumbuliwa na tatizo la kiafya na saikolojia.


Aliwapongeza taasisi ya Dnata na kituo cha Barefoot kutoa elimu ya masuala ya viungo vya uzazi vya mwanamke, hedhi salama kwa lengo la kuepusha tatizo la mimba za utotoni, magonjwa ya zinaa na kujitambua.

Aidha Bi maryam, aliwataka wanafunzi wa skuli ya kijini, kutumia vizuri vifaa na elimu waliopatiwa ili kuwa afya bora sambamba na kuwapatia elimu hiyo wanawake wengine kufikia ndoto zao.

Sambamba na hayo aliwasisitiza wanafunzi kuwa majasiri na kujikita katika masomo na kupinga udhalilishaji wa kijinsia ili kufikia ndoto zao za kuwa viongozi bora. 

Nae Mkurugenzi Miradi kituo cha kinamama cha umeme wa jua Zanzibar (Barefoot) Brenda Geofrey Ndossi alisema, lengo la kugawa vifaa hivyo ni watoto wakike kuhudhuria masomo yao kwa wakati na kujiamini wakati wote.

Aidha alisema kwa kushirikiana na Dnata, wameona haja ya kuitumia siku ya wanawakwe duniani kutoa elimu na kugawa vifaa kutokana na umuhimu wa afya na kujikikinga na maradhi mbali mbali ikiwemo afya ya uzazi.

Sambamba na hayo aliwataka wanawake kupambana na kujifunza vitu vingi zaidi ili kupata ujuzi na maendeleo nchini.

Awali Mratibu Afya ya mama na mtoto wilaya ya Magharibi B, Safia Khamis Juma, aliwasisitiza wanawake kula vyakula vya bora ikiwemo mboga za majani na matunda ili kuimarisha afya zao kwani wanapoteza madini ya chuma kila mwezi.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa skuli ya kijini, Bahati Faki Omar, alisema wamefurahishwa kupatiwa taula za kike kwa ajili ya hifadhi, awali walitumia vitambaa vya kawaida.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI