WANANCHI ZANZIBAR WAPONGEZA UONGOZI WA DK SAMIA.
NA MWANDISHI WETU, UNGUJA. WANANCHI wa Zanzibar wamesema,Tanzania wamepata kiongozi ambae Taifa likimuenzi wataweza kuendelea kupiga hatua mbalimbali za kimaendeleo na hatua bora zaidi. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati mbalimbali, wananchi hao wamesema, uongozi wa Dk. Samia umekuwa ukiwashirikisha wananchi wote ambapo ni sifa pekee ya kiongozi aliyekuwa bora na anapaswa kuenziwa na taifa. Mmoja ya wananchi hao, ambae ni mzee wa maskani ya kachorora, Mohamed Mussa Seif (mkobani) alisema, endapo kiongozi huyo akiendelea kupewa ushirikiano maendeleo zaidi yatapatikana kwa wananchi ikiwemo kuwanufaisha mmoja mmoja. Alisema, Dk. Samia, amekuwa akitambua changamoto mbalimbali za wananchi kwani uongozi wake umetokea chini na alikuwa bega kwa bega na watu na ni mpenda maendeleo na hana ubaguzi wa dini, chama wala rangi ya mtu. Hivyo, alisema utendaji wa kazi wa Rais. Dk Samia hauna shaka kwani ni kiongozi mzoefu na mwanamapinduzi wa kweli na mpenda haki kwa watu...