UKOSEFU WA MALEZI YA BABA YAELEZWA KUCHANGIA NDOA ZA MAPEMA PAMOJA NA MIMBA ZA UMRI MDOGO KWA WATOTO WA KIKE.

NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA. 


WAZAZI WENGI WAKIUME WAMEKUWA wakiwekeza nguvu zao zaidi kuwashughulikia Watoto wanapokuwa Wadogo  lakini  akifikia Kuanzia Miaka 13 na kiendelea tu bhasi nguvu za kuwashughulikia katika Malezi zinaanza kupungua wakati kuanzia Umri huo   ilipaswa Usimamizi Uongezeke Mara Mbili Zaidi  kwa Watoto wakike Na Wakiume mana Mabadiliko Ya Tabia huanzia Hapo".
 
Hayo Ni maneno ya Nadhira Khamis Iddi Ambae Nadhira Khamis Iddi aliyezaliwa katika kijiji cha Mgogoni Konde  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, mwenye umri wa miaka 21 kwa sasa ni Mama na Mlezi wa Watoto wake wawili wa Kiume aliowapata katika Mwaka 2017/ 2019 Iliyopita baada ya kupewa ujauzito na kuozeshwa Mume  akiwa na umri wa miaka  16.

Nadhira ambae alizaliwa mwaka 2003 kwa sasa anaishi Mjini Chake Chake akiwa na wanawe hao pamoja na wazazi wake wote wawili baba na mama ambao walihamia miaka mingi iliyopita.

Nadhira ambaye alisema katika skuli ya sekondari Shamiani hadi kidato cha 3 katika Mwaka 2017 ambapo mwishoni  kidato cha tatu hafla alipewa taarifa na Wazazi wake kuwa alitokea mume aliyeomposha kwa ajili ya kufunga nae ndoa  na tayari walishampokelea mahari kwa ajili ya kutolewa. 

Jambo hilo lilimkosesha amani    kumpatia msongo wa mawazo na kupoteza hamu ya kusoma kama aliyokuwa nayo awali kwani suala la ndoa kwa wakati huo halikuwa moyoni na chague lake ilikuwa ni kusoma.

 Anawataka Wazazi  Wote Nchini Kusimamia Vyema Malezi ya Watoto wakike  zaidi  wanapofikia Umri wa Kubaleghe  (Kuvunja Ungo) ili Kuwaepusha na ndoa za Mapema Pamoja na Mimba za Umri Mdogo ambazo hupelekea Kupata Athari mbali mbali  na kuacha changamoto za Kiafya pamoja na  Maisha yao. 

 Aliendelea Na Masomo bila Malengo yeyote kwa Vile Tayari Baba yake  alikuwa akisubiria  binti yake huyo amalize  Elimu ya Lazima na Kutimiza Adhma yake hiyo ya kumuozesha Mume Ambae Alikuwa ni Mtoto wa Rafiki Yake Wa kushibana. 

 Nadhira Hakuwa  tena na Shauku Juu ya Kuendelea na kusoma  wala kuolewa na Mtoto  huyo  ambae  licha kuwa alikuwa ni Chaguo Sahihi  kwa Baba yake kutokana na Urafiki waliokuwa nao Wazazi wao lakini   Hakuvutiwa nae. 
 
" Wakati ule Nilikuwa Sijui hata Nataka kitu Gani, Mana nilikuwa nikenda Skuli naona Hata nikisema nisome Mwisho wa siku Nyumbani Baba yangu anasubiri  Nimalize  Skuli tu Niolewe, Nikijiangalia Mume wenyewe Simtaki yani Umu Rohoni mwangu Nilikuwa Namchukia Hata kama alikuwa hana Tabia mbaya yeyote ile". 


"Kila nilichokuwa nakifanya Nilijihisi Kazi bure tu mawazo mbali mbali yalinijia kwa wakati ule, Nilikuwa najifikiria niache Masomo  Nitoroke  Nyumbani watu Wasinione Au nifanye nini Mawazo kichwani kwangu yalikuwa yanagongana Kiukweli nilikuwa Sipo Sawa kabisa"Alisema Nadhira. 

 Umri wake Ulikuwa Bado Haukuwa  sahahihi wa kufanya maamuzi ,  Lakini Pia Kipindi ambacho Mawazo  na Ushauri kutoka kumdi rika Nduo pekee yalikuwa yanapata Nafasi ambao ni Wanafunzi Wenzake pamoja na Marafiki Mtaani kwao. 

 Haikuwa Rahisi kwa Mtoto Mwenye Umri wa Miaka 16 kuamua Maamuzi yenye kueleweka, Badala yake Maamuzi mabaya ambayo yamepelekea kuharibu ndoto zake zote Alizojiwekea za kuwa Mwalimu baadae zikiishia Ukingoni. 

BABA WA NADHIRA NI MTU WA AINA GANI KATIKA  MALEZI YA WATOTO! 

 Mara nyingi Baba Mzazi wa Nadhira Alikuwa   Hashindi Nyumbani kwake siku nyengine Akiishia kulala nje Kabisa na Nyumba yake Kutokana na kazi zake  anazozifanya   za Kuongozana na Mafundi  Ujenzi  Nyumba Pamoja na Kupaka rangi katika Majumba. 

 Shughuli hiyo Humfanya  Mzee Khamis  kutoka Nyumbani kwake Mapema na Kurudi Usiku Akiwa Amechoka , Huku  ikiwa ni Mara Chache  pekee hurudi Mapema. 

 " Baba yangu Alikuwa hana muda wakujua chochote  kwa Watoto na Mama yangu Mimi Alijitahidi kunipambania Nisome Kwa vile nilikuwa nalalamika sana Sitaki Kuolewa Lakini Nguvu yake ilikuwa ni ndogo Kutokana na kile Ambacho baba yangu Alishakiamua  Alikuwa anafuata tu Amri hana tena kauli yeyote ". 

"Naendelea Kujuta juu ya Maamuzi yangu niliyoyachukuwa ,  ya kumdanganya mama yangu Bikhadija  Nyumbani yakuwa naenda Skuli kumbe Siendi".

WITO KWA JAMII. 
 
Nadhira anatamani Wazazi wote walichukue hili ambalo limemkuta yeye  kuwa funzo katika kuwalea watoto wengine  wakike  kwa kuongeza Ufuatiliaji pamoja na Ulinzi  Ili kuweza kujua Mienendo na Tabia zao. 

 "Ni lazima Wazazi  wajue Mtoto wakike anacheza wapi, na nani muda gani  mtoto wakike akifikia umri wa kuvunja ungo anahitaji ulinzi mkubwa kutoka kwa Baba  nathubutu kusema zaidi ya alipokuwa Mchanga Kwa sababu  Alipokuwa mchanga Mama peke yake Anamuweza lakini umri wa kupevuka Mama anashindwa peke yake  baadhi ya Watoto wakike  Umri ule wa mwanzo  mwanzo baada  kuvunja ungo  wanapelekeshwa na Mihemko ya Kimwili huku akili na maarifa bado hawana wanaambulia kudhalilika   ndio ambayo yalinitokea mimi ". 

 Niliamua Kuacha Skuli kwa Zaidi ya Miezi Mwili, Huku wazazi wangu Wakiamini mimi Bado Naenda skuli na kurudi kwa vile Nilikuwa natoka na Madaftari,  Siku ambazo nilikiwa nachelewa kurudi   Mama yangu Nilikuwa namuambia  Tumeambiwa Tubakie  Tusome Masomo ya Ziada Anaamini Tu. 

"Wazazi wakiendelea kunisubiria nimalize Darasa la 12 wanipeleke kwa Mume Na mimi nikaona isiwe Tabu Boraniache Skuli,  Nikapata Ujauzito kwa Mwanaume Ambae Yeye Alikuwa ni Rafiki yangu Huko Skuli Yeye Akiwa Darasa la 12 na  Mimi Darasa La 12Tofauti yetu yalikuwa ni Madarasa tu".

"Mama yangu wala Baba yangu wote Hawakugundua  kuhusu mimi kukatisha Masomo wala kuhusu ujauzito Mpka Pale Ambapo Mabadiliko ya Mwili wangu yalipoanza kujitokeza,  huku Taarifa za mimi kutoonekana Skuli Zikifikishwa nyumbani kwa Barua kutoka kwa Mwalimu wa Darasa aliempa Mwanafunzi mwezangu Barua ya kuipeleka Nyumbani. 

" Mwili wangu Ulikuwa Umevimba Sana  Hususan Miguu na Maziwa Kiasi ambacho Kila Aliekuwa Ananiona ananishangaa na kunitilia Mashaka Ndipo mama yangu Alipoamua kuniuliza kwa ukali  kuhusu ujauzito mimi nikiwa napinga na kukataa  kwa Msisitizo  huku nikijiaminisha kuwa Sina Ujauzito licha ya kuwa Nilikuwa nimefanya Mapenzi na Mwanaume Ambae ni mwanafunzi mwezangu kwa Zaidi ya mara Kadhaa". 

 Waswahili Wanasema  "MAJI YAKIMWAGIKA HAYAZOLEKI"

  "Nililazimika Kuanza Maisha ya ndoa nikiwa Bado Mdogo, nikakatisha Masomo Darasa la 12  licha ya kuwa mwishoni  Kumalizia Elimu yangu hiyo iliyokuwa ya Lazima kwa kuepusha Aibu na mvutano wa Familia uliojitokeza baada ya kuoatwa na mitihani hiyo".

NADHIRA AMEKUMBANA NA CHANGAMOTO GANI KATIKA AFYA YA UZAZI! 

"Nilijifungua Mtoto wangu wa kwanza Kwa Shida na maumivu ambayo niliyahisi siyo ya kawaida Maishani mwangu, Na Changamoto ya Kiafya Ilianza hapo  kwa sababu Tangia Siku hiyo Mpka mtoto wangu   Alifikisha miezi Tisa Mimi nilikuwa natokwa na Damu nyingi  kila siku ikitokea nimepumzika bhasi ni Siku moja tu yapili Inaendelea Kunitoka katika Sehemu Zangu Za Siri". 

" Kama hiyo haitoshi Nilikuwa naumwa na Tumbo Sana mara kwa mara, Pamoja na Miguu yangu kuishiwa na Nguvu Kiasi ambacho kutembea mwendo mrefu kidogo kwangu  ilikuwa Shida ". 

 " Nilipokuwa nafika Hospitali juu ya Tatizo hilo Dakatari aliniambia sio Tatizo  Ni donge la Damu ambalo wakati najifungua halikumlaiza kutoka niliwache Litoke kidogo kidogo Mpaka Pale litakapomalizika wenyewe,  Wakati  awali Daktari wa kwanza kukutana nae Nilipomuahdithia Bila kujua kama nilikuwa nimejufungua Mtoto Alinipima na kuniambia kuwa Nimeharibu Mimba ndio sababu iliyonifanya nitokwe na Damu Mapande kwa Mapande jambo ambalo halikuwepo". 

 Mpka sasa bado Napata maumvu ya Mguu kila  inapofika kipindi cha baraidi kama siku hizi Na maumivu Makali, Jambo ambalo huenda kama sio kujifungua Nikiwa na Umri Mdogo lisingeweza kunitokeza  "

 WATAALAMU WA AFYA WANASEMAJE JUU YA SUALA HILI NA JEE NI UPI  UMRI SAHIHI WA KUBEBA UJAUZITO NA KUOLEWA !. 

Ibrahim Said  Ibrahim Ni Dakatari  Wa Magonjwa ya kina Mama  katika Hospitali ya Wilaya Chake Chake Alisema kuwa Muda Sahihi kwajili ya Kubeba Ujauzito ni Kuanzia Umri  20 hadi 40 ambapo amesema chini ya Umri huo  Sio Sahihi kutokana na kujitokeza   changamoto Mbali mbali. 

" Kuna Athari nyingi za kiafya zinazotokana na  Ndoa pamoja na Mimba za Umri Mdogo ambao ni chini ya Miaka 20, kwanza ni kupatikana kwa Maradhi ya Kifafa cha Mimba,  Maradhi ya Mfumo wa Damu, Mimba kuharibika Kuzaa Watoto ambao Njiti,  hao ni watoto ambao huzaliwa kabla kufika Miezi Tisa. 

"Matatizo ya Afya kwa Muda Mrefu, Ugumba, Kutokwa na Damu nyingi, Mwili kupungua Uzito kubwa kuliko yoto Ni Vifo vya Mama Wajawazito  na hii ni kutokana na Viungo vya  Mwili kukosa Matayarisho yaani havijakomaa kubeba ujauzito,lakini pia  Hupelekea kupatikana kwa Mimba zisizotarajiwa  na hatimae kupelekea Maradhi mbali mbali  katika Afya ya Uzazi. 

 Mimba Kuanzia Miaka 15 hadi  19 mara nyingi inakuwa hata yale maumbile ya  na Fuko la kuhifadhia Mtoto linakuwa bado halijajishika vizuri kutokana na Umri huu mara nyingi Watoto wakike ndio Wanavunja ungo na kupata Damu ya Hedhi. 

 Kiumbe kitakachobebwa mara nyingi   kinakuwa dhaifu, Viungo vya uzazi vinakuwa  vidogo kwaio Atahari zote hizi mara nyingi zinajitokeza kwa Wale Mama ambao wanabeba ujauzito Chini ya umri Unaofaa kitaalamu ni Wachavhe sana Ambao hupata changamito hizi wanaopata Changamoto hizi Endapo wataolewa kwa Muda Sahihi ambao unaruhusiwa Kubeba ujauzito. 

 Baadhi ya Wazazi Ambao Walizungumza na Mwandishi wa Makala hii Akiwemo Hadija Juma Ali pamoja na Muhammed Heri Rajab wamesema Changamoto za Mimba za Umri mdogo na ndoa za Mapema  zinatokana na Wazazi kushindwa kusimamia Majukumu yao Ipasavyo, tamaa jambo ambalo na hupelekea Kuharibu  Afya  na ndoto za Watoto.
Njia Bora  ya kulinda Afya ya Uzazi kwa mama na watoto Ili kuepusha Atahari zitokanazo na Mimba za Umri mdogo Pamoja na Ndoa za Mapema ni Kusimamia vyema Malezi ya Watoto wakike Pamoja na kuwapa Elimu itakayowawezesha kujitambua na kuwasaidia kujilinda na kudhibiti Ndoa za Mapema Lengo ikiwa ni kupunguza  Vifo vya Mama na Watoto ambavyo vinaendelea kuongeza Siku hadi Siku. 
Kwa sasa Nadhira anaendelea kufanya kazi za Nyumabani kwake  akiendelea kuwalea watoto wake huku na  Mumewake akimuahidi Maisha na Malezi bora ili watoto wao Wasije kukumbana na Changamoto ziliwapata wao na kupelekea kuishi Bila ndoto zao Zilizokatika kutokana na Ndoa za  Umri Mdogo. 

Mwisho 

Mwisho. 





 












 







 



 

 

 



 






  

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI