HOSPITALI 10 ZA JENGWA UNGUJA NA PEMBA UONGOZI WA AWAMU YA SITA.
NA MWANDISHI WETU, UNGUJA
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya, imesema kupitia fedha za UVICO 19 zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Dk. Samia Suluhu Hassan zimejenga jumla ya hospital 10 katika wilaya ya Unguja na Pemba na hospitali ya mkoa moja iliyokuwepo Lumumba Mjini Unguja.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisini kwake Mombasa, Afisa kitengo kinachosimamia mradi wa ujenzi wa hospitali na miradi yote ya ujenzi wizara ya Afya Zanzibar, Amina Habibu, alisema, hospitali hizo zitakuwa zinatoa huduma mbalimbali ikiwemo za mama na watoto.
Alisema, ujenzi wa hospitali hizo zimekuwa zinakwenda vizuri na nyengine zimeshafunguliwa na huduma zinaendelea katika hospitali jambo ambalo limewarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma zilizokuwa bora na muhimu.
Alisema, kupitia fedha hizo wizara zimenufaika ambapo hivi sasa wamekuwa wakitoa huduma nyingi ikiwemo za dharura.
Aidha alisema kabla ya ujenzi wa hospitali hizo wananchi walikuwa wakipata shida kufuata huduma za afya katika hospitali ya rufaa ya mnazi mmoja jambo ambalo lilikuwa linasababisha pia kuengezeka kwa vifo.
Hivyo, alisema kukamilika kwa hospitali hizo wananchi wamekuwa wakipata huduma hizo kwani zimekuwa zikitolewa kwa masaa 24 kwani zimekuwa zikitoa huduma za dharura na maradhi mengine mbalimbali.
Alisema katika hospitali hizo, zimekuwa na vifaa mbalimbali na maabaraza za kisasa ambapo wamekuwa wakichunguzia maradhi mbalimbali huduma za mkono kwa mkono.
"Hospitali hivi ni za kisasa hata data zetu huwa tunazipata kwenye mfumo maalum, usajili wa mahudhurio kwa kweli hospitali hizi ni za kisasa kwani zinatumia teknolojia za kisasa" alisema.
Alifahamisha kuwa hospitali hizo zimekuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 100 kwa siku huku akisisitiza kuwa zimekuwa na vifaa tiba zilizvyokuwa bora, hivyo, aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwani wananchi wamekuwa wakipata huduma zilizokuwa bora.
Sambamba na hayo alipongeza viongozi wakuu wa nchi kwani wamekuwa wakitekeleza maendeleo kwa vitendo na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa awamu.
Nao, wananchi wa Zanzibar wamesema uwepo wa hospitali hizo zimewarahisishia kwenda katika hospitali ya rufaa ya mnazi mmoja ambapo katika hopsitali hizo wamekuwa wakipata huduma hizo kwa urahisi.
Rehema Hassan Nahoda, kutoka Muungoni, alisema, hopsitali ya kitogani imekuwa ikitoa huduma zilizokuwa bora na matibabu yake yapo masaa 24.
Hivyo, aliwapongeza viongozi wakuu kwani wamekuwa na jitihada mbalimbali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizokuwa bora ikiwemo matibabu.
Sambamba na hayo, alisema wataendelea kuwaunga mkono viongozi hao kwani viongozi wa awamu ya sita na ya nane wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu.
Comments
Post a Comment