RAIFFA ABDALLA MAKAME KIJANA ANAENDELEA KUTIMIZA MALENGO YAKE KUONESHA UTHUBUTU, SAMBAMBA NA KUJIVUNIA MAFANIKIO KUPITIA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII AWAASA VIJANA KUTUMIA FURSA



Na, Amina Ahmed Moh’d - Pemba     (0719859184) (minnah1202@gmail) 

"SIKU ZOTE NAWAAMBIA  Vijana wenzangu Unaweza kuwa Yue ambae unataka kuwa Lakini Anza Sasa, Siri ya Mafanikio Peke  ambayo Duniani kote Ao mabilionea  namba moja   siri yao kubwa Nikuanza hakuna siri nyengine hawakuwa tu Mabilionea kwa kulala tu na kuamka". Ni Maneno ya Raiffa Abdalla Makame Mwanamke alietimiza ndoto zake  Kupitia fursa za Mitandao ya kijamii.


 "Nikiwa kijana Ninandoto ambazo nimejiwekea  na furaha yangu kubwa ni kuona Zinaendelea kutimia siku hadi siku, Na zinatimia kwa Sababu Ya Utayari wangu katika kufikia Malengo niliyojiwekea, Umakini, Kujifunza kwa wengine sambamba na kutumia Fursa  zilizopo mbele yangu "Aliendelea Raiffa. 


JEE RAIFFA NI NANI! 

Jina Lake kamili ni kama ambavyo limesimuliwa huko juu, Ni Mtoto wa Pili kati ya watoto wa 5 wa Mzee Abdalla Makame Na Mke wake Bi Tatu Omar Juma,  Wakaazi wa Fuoni Taveta Wilaya ya Magharb B Unguja. 

   (  MC GOLDEN VOICE )  ni jina maarufu Ambalo Anatumia Raiffa Katika  mitandao ya  kijamii ambapo  anaendelea kufanya shughuli zake  mbali mbali kwa usahihi na kujipatia Kipato.

 Kama hiyo haitoshi Raiffa pia ni Mwanafunzi  wa  shahada ya Mawasiliano  ya Mawasiliano ya Umma Katika Chuo kikuu cha Zanzibar ( Z. U) Mwaka Wa Tatu, Ambapo awali alimaliza Elimu yake ya kidato Cha Sita katika Skuli ya Sekondari Philter Federal Shool  Dar - essalam mwaka 2019.

 Mzee Abdalla makame pamoja Tatu Omar omar Juma  hawakupata bahati ya kumlea Mtoto wao kutokana na sababu Zilizokuwa njr ya Uwezo wao na kulazimika kulelewa na Walezi wake ambao Ni Mwanjabu Muhammed.

Akiwa Mdogo Darasa la Tisa Raiffa  ndoto yake kubwa ni kuwa Mtangazaji maarufu  katika Shirika kubwa La Utangazaji Duniani Linalojulikana kwa jina La British Broadcasting Corporation    (BBC)  ugumu kwake ulibakia kuwa Wapi wataanzia kufika apo anapopataka, jambo ambalo Mlezi wake Bi Mwanjabu alikuwa anampa moyo ya kuwa upo uwezekano mkubwa wa kutimiza ndoto yake Hiyo. 

           RAIFFA ABDALLA MAKAME  -  MTANGAZAJI 

"Mlezi wangu Alikuwa Ananipa moyo sana juu ya kutimiza ndoto yangu hiyo, alitumia fursa hiyo kila ambapo inatokea nafasi  Nyumbani kwetu alikiwa ananikumbusha,  ulisema unataka kuwa mtangazaji Haya njoo hapa utangaze, ni kweli nilikuwa nachukua kipaza sauti katika sherehe zinazotokea nyumbani nakaribisha Wageni safari yangu ya kutangaza kidogo kidogo ilianza hapo" 

 "Hamu na shauku yangu ilizidi kuongezeka juu ya ndoto hiyo ya kutaka kuwa mtangazaji  kila siku huku Tatizo kubwa likibaki kichwani mwangu Vipi nitafika BBC dunia Iweze kunitambua na kuona kipaji changu,  sikujua nianze wapi, kiukweli licha ya kuwa n a hiyo ndoto lakini pia Nimejaliwa kipaji cha kuzungumza kwa kujiamini mbele ya mtu yeyote na mahala Popote  bhasi niliendelea mpka nilipomaliza Skuli Msimamo wangu ulikuwa huo huo " 

 Matumaini ya Raiffa  (MC, GOLDEN VOICE)  kabla ya kuingia Chuo kikuu  2020 Ni kuona Ushindani mkubwa kutoka kwa wanafunzi wenzake ambao wanasoma Fani ya aina moja  Chuonihapo, Lakini mambo yalikuwa tofauti Mara tu baada ya  kufika Zanzibar University ( Z. U

"Hakukuwa na Ushindani  wa aina yeyote pale chuoni kutokana na waliowengi ambao tulikuwa tunasoma  Fani moja ya Mawasiliano ya Umma kujikita zaidi, katika masuala ya Kuandika, Kupiga Picha  na sio Kutangaza  Wengine Walikuwa wanataka Kuwa Watu wa kazi maalum ofisini tu hwapo kabisa nilipo mimi,sio wanawake wala wanaume hawakuwa na ushindani Mkubwa katik kutangaza. 


        ALIWEZAJE KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUPATA MAFANIKIO NA KUTIMIZA NDOTO ZAKE! 

"  Kiukweli ni kwamba Mitandao ya kijamii kwa wanawake lakini kwa vijana wote inafursa nyingi sana, Tunapozungumzia  masuala  mazima ya kuonsha uwezo wowote mtu alikuwa nao kwa Watanzania lakini hata wasio uwa watanzania bhasi mitandao ya kijamii ndi suluhisho pekee ambalo mtu anaweza  kutumia kuomsha kila alicho nacho. Anasema Raiffa. 

"Binafsi Mimi nilianza tu Baada ya kumaliza Kidato cha 6  na kuingia chuo 2020 Hapo ndipo Rasmi nilianza kutumia mitandao ya Kijamii, Kwa Kutumia simu Janja  Nakumbuka mwaka wa Kwanza Muhula Wa Kwanza  niliona Nisikae tu bure bure wakati ninadoto kichwani,wakati uo  Ndugu Muandishi kumbuka apo Ndio nimetoka Moja kwa moja kutoka skuli sijui Lolote juu ya masuala ya Kutangaza. 

                MC GOLDEN,  RAIFF ABDALLA 

 "Lakini nikasema  sawa Mimi naweza na nitafanya, wacha niendelee kupambana, Bhasi niliona nisikae tu bure bure Nisubiri kupata kilakitu chuoni, nikasema Bora nianze kivyovyote  vile mimi bora nianze  nikaanza kwa kujitolea katika runinga moja inaitwa Haiba Tv, Ni Tv  ya Online ambyo inajihusish na mambo ya kutangaza utalii". 

"Nilienda Pale nikapokelewa vizuri na Uongozi, nikawaeleza dhamira yangu nikajitambulisha mimi ni nani na nataka nini  na uzuri ni kwamba naweza kujieleza, hawakunitilia ugumu walikubali kwa sababu kiukweli ni vijana wachace wanawake hapa kwetu Zanzibar kuwa na utayari juu ya masuala ya kutangaza wala kuzitumia fursa hizi".

Bhasi pale nilianza kujifunza nafundishwa namna ya kutangaza, namna gani ya kukaa mbele ya kamera, nafundishwa wapi nipunguze sauti wapi nipandishe wapi niongee kwa nguvu  nikawa nafanya mazoezi kwa nguvu zangu zote. 

 "Wakati ukafika sasa nikaanza kupewa vipindi nitangaze, nitie sauti hapo  sasa ndipo nilipokuwa na shauku ya kutaka kuwaonesha watu nafanya kitu gani nikawaza nikasema bora hizi kazi zangu nizichukue nizihifadhi katika simu yangu, nikawa nawaomba wakimaliza  wanirikodie wanipatie mwenyewe kike ambacho nimekifanya au kukitangaza. 

" Hapo sasa nikawa nachukua ivo ivo vipande naweka kwenye statas watu wajionee, wakawa wanaangalia wanatoa mrejesho wapo waliokuwa wananipa hongera wapo waliokuwa wananikosoa  wengine wananipa moyo, Lakini ikawa najiuliza  nitaviweka mpaka lini kwenye simu yangu ikiharibika jee, Nikasema Bora nianze kuvituma katika mitandao na Safari ya kutumia mitandao ya kijamii rasmi ikaanzia hapo. 


"Nilianza kufungua Accaunt  na kutengeneza Utambulisho wangu katika mtandao wa Facebook, instagram  nikaweka jina langu halisi Raiffa Abdalla Makame na kujiwekea jina la umaarufu Nikaandika  (MC GOLDEN VOICE ) Nikawa natuma zile kazi zangu ambazo nilikua nazitangaza pale haiba Tv online  vipindi mbali mbali, kama vile Durua ya msamiati, na ikawa nahamasika najirikodi mwenyewe  kama natangaza, Siku nyengine nawaambia wale Wasimamizi wanirikodi kama  natangaza  kweli, baadhi ya muda najirikodi mwenyewe kwa simu yangu natuma kwenye acaunt Napokea  Maoni kwa watu wanaona wananipa mrejesho wengine watangazaji wakubwa kabisa duniani na Tanzania hii"Alisema. 

Anaendelea na Kusema kuwa"Kupitia Mitandao ya kijamii imekuwa rahisi  kuwafikia  Watu wengi mashuhuri,  Ndani na nje ya nchi ambao na wao wapo katika fani kama ya kwangu ya uandishi wa habari, kikukweli muitikio wa watu juu ya ile kazi zangu ambazo nazituma, naweza kuonhea nao na ukunishauri maendeleo katika kukuza taaluma na ndoto zangu. 


 Takwimu za Ripoti ya Utendaji wa Sekta ya Mawasiliano Nchini Tanzani TCRA  iliyotolewa Tareh e 25 Mwezi wa  10  mwaka 2022  zilibainisha kuwa   jumla ya Mitandao (5) ya kijamii  inatumiwa kwa Wingi Zaidi  Nchini Tanzania  Mitandao hiyo  ambayo ni    Facebook, Instagram, Whasap, Tik tok, pamoja na  Youtube. 

Bila shaka Msomaji utakuwa unajiuliza  Maneno ya Lugha ya kigeni  Ambyo sio kiswahili katika  makala hii imekuwaje! 

Lakini  nikutoe wasiwasi, ya kuwa Ugeni wa lugha katika makala hii ya kiswahii juu ya Mitandao hiyo maarufu umelazimika ni kutokana na kukosekana uhalisia wa Tafsiri halisi iliyokusudiwa katika Majina ya Mitandao hiyo hivyo Neno lolote Ambalo litatumika katika Makala hii likiwa neno la lugha ya kigeni Msomaji wa Maala hii Elewa ya kuwa Imelazimika, ni kutokana na kukosa mbadala wa maneno hayo. 

 Hivyo maneno kama Whasap, Instagram, Facebook, Tik tok, Smart phone, Internet, Account, Mc, Golden voice na mengineyo Yamelazimika kutokana na kukosekana ushahihi   uliokusudiwa endapo  yatatumika katika  Lugha ya Kiswahili na kukukwaza wewe Msomaji wangu wa makala hii yenye mazingatio kwa vijana na wazee pia. 

Ili kuifikia Mitandao hiyo Mpendwa msomaji  mtumiaji  yeyote, atalazimika Kuwa Na simu Janja,Smart phone  au mbadala wa kifaa chengine, ambacho kinauwezo wa kufikiwa na huduma ya intaneti. 

Kwa mujibu wa  Ripoti hiyo  ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TCRA  ilieleza kuwa Watumiaji wa Simu janja   Tanzania ambazo zinauwezo wa kupokea huduma za intaneti  na kuweza kuifikia mitandao ya kijamii wameongezeka kutoka 29,169,958 Juni 2022 hadi 31,122,163 Septemba 2022 sawa na ongezeko la asilimia 6.7%  ukilinganisha na miaka 5 iliyopita .  

Takwimu hiyo ya TCRA ilibainisha kuwa kati ya mitandao hiyo mitano (5) ya kijamii  imefikiwa zaidi na kifaa kimoja ambacho simu Janja, ikifuatiwa na  ,komputer mpakato,  pamoja na kiskwambi,na komputer ya mezani.

                MAFANIKIO YA RAIFFA  MC GOLDEN VOICE

 "Nikiwa naendelea na Masomo huku naendelea na Shuguhuli za utangazaji Haiba Tv, na kupost nikaanza kupata Fursa za kuwa Mshereheshaji katika  shererehe mbali mbali, Watu wananitafuta kupitia Mawasiliano yangu niliyoyaweka , Wengine Wananifata DM huko katika instagram , wananiambia Tunahitaji uwe mshereheshaji katika Shughul yetu Tunakubaliana na mimi naenda , nakuwa MC  katika Mikutano mbali mbali, Na huko nazidi kujifaragua Najitangaza pia Nikimaliza shuguli napost Instagram ".


" KWAVILE Uongozi na Wanafunzi wote Pale  Z. U Walijua nini Raiffa Anahitaji bhasi Na wao walikuwa wananipa fursa zinazokuja pale Chuoni zinazohusiana na kutangaza, Namimi nazitumia, Najipatia kipato kupitia kazi hii ya Utangazaji katika mashuhuli mbali mbali nkidhi mahitaji yangu. 

 " Kupitia Mitandao ya kijamii, siku moja baada ya  kupost makala yangu ambayo nimeifanya pale Haiba Tv inayohusu michezo, kwa bahati njema  nilipokea Simu kutoka kwa Mtangazaji mmoja wa BBC akanipongeza akanishauri lakini mwisho akaniambia kwamba anataka nishirikiane nae katika  Makala za Michezo  BBC Radio, Nilifurahi sana na baada ya wiki nikaanza kushirikiana nae kufanya kazi, nikawa natia sauti Makala za Michezo katika kipindi cha radio cha BBC kila jumapili  saa 3 usiku Kipindi kinaitwa Michezo na wachezaji Nasikika humo  Nikiwa kama Ripota kutoka Zanzibar Na najipatia fedha nakidhi mahitaji"

"Niliona Ndoto yangu inatimikidogo kidogo sababu naamini Kuna siku Nitafika Pale ambapo Zuhra Yunuss na Salim kikeke Walikuwa Nitaangaza Pale Dunia itazidi kunifahamu na naamini kwa sababu Nimeshaanza kupata mwanga Leo niko rafio BBC kesho nitakuwa Mtangazaji BBC Tv ". 

" Mkononi mwangu Tayari nina Tunzo Kubwa Mbili Ambazo zote hizo Kupitia Mtandao wa Kijamii wa Instagram Nimezipata 'Mtangazaji bora Wa kike Vyuo vikuu Vyote Tanzania 2021,  katika Mashindano ya University awards,

 Mtangazaji na Mwandishi  bora katika Tunzo za Ladies Talk Tanzania 2022 Zote hizo niliweza kupigiwa kura katika mitandaoya kijamii zaidi instagram ni baada ya kuweka kazi zangu na kushindanisha na kazi za wengine licha ya kuwa na tunzo pia Ninapata fursa ya kushiriki nafasi mbali mbali zinazoemdelea kunijenga zaidi katika fani yangu  ". 


nimeweza kufanya kazi na watu wakubwa sana Ukiachilia mbali BBC Nimekuwa balozi wa makampuni mbali mbali, nimezungumza na watu ambao isingekuwa mitandao ya kijamii nisingeweza  kuwafikia  hata siku moja, Kina Shafii thedone na wengine, Napata Matangazo katika Taasisi mbali mbali kuyaweka sauti na kujipatia kipato,  Nimepata umaarufu Kupitia kazi yangu hiyo yadoto zangu. 

 Nina mwaka wa Tatu saivi katika masuala ya utangazaji lakini mafanikioni makubwa makubwa  zaidi ya nilivyofikiria na hii imetokana na umakini wa kutumia frsa katika Mitandao ya kijamii. 

    JEE! WATU WANAOMJUA WANAMZUNGUZIAJE  RAIFFA

 Tatu  Omar  Juma ni mama Mzazi wa Raiffa anasema mafanikio ya mtoto wake anayoyapata kupitia mitamdao ya kijamii imekuwa chachu ya kubadilisha Mtazamo wake ambao alikuwa nao juu ya mitandao ya kijamii kwa watoto wakike, huki Baba yake akisema kuwa furaha na moyo wa kumuunga mkono binti yake katika kufikia zaidi mafanikio inazidi kuongezeka siku hadi siku kila anapoona na kusikia mtoto wake anatwaja katika midomo ya watu kwa wema. 


 Naila Mcha haji pamoja na  Mwajuma Zaidu Makame wakisema kuwa wanaendelea kujifunza ujasiri na uthubutu alionao dada yao katika kupigania  na kutimiza ndoto zake. 

Riziki  Abdalla khamis Ni Msemaji wa bunge katika chuo kikuu Cha Zanzibar University anasema Uwepo wa raiffa chuoni hapo umekuwachachu kubwa ya kuongeza hamasa kwa wanafunzi wengine  kuipenda fani ya utangazaji Huku wakiendelea kuiga mambo mazuti kutoka kwake. 

Mwanjabu ambae ni Mlezi wa Raiffa Anasema Aligundua uwezo mkubwa alionao Raiffa kutokana na kujiamini akia mdogo licha ya kumsaidia umuonesha njia ya mafanikio hayo lakini awali hakuwahi kufikiria kuhusu kushinda Tunzo mbali mbali Mtoto wake. 

WITO GANI KWA VIJANA JUU YA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUTIMIZA NDOTO ZAO. 

Changamoto zisiturudishe nyuma sisi vijana mimi wapo ambao walikuwa wananiambia nimeaza kuwa muhuni najituma mitandaoni, lakini ka vile lengo langu nilikuwa nalo nilipuuza ayo maneno, Vijana wenzangu hususan watoto wakike kuna fursa nyinyi katika mitandao endapo tutakuwa makini kuitumia ipasavyo mitandao hiyo. 


"SAFARI NI HATUA ILI UIFIKE INAKUBIDI UIANZE yeyote mwenye kuhitaji kutimiza malengo yake asiogope kuanza Dunia sasa imeelekea Kiganjani, Hivyo hata fursa nazo zipo uko, Ukiwa mfanya biashara unaweza kutumia mitandao kujitangaza, ukiwa mwalimu, Ukihitaji kusoma, Kuiga mambo mazuri, kuwafikia watu kwa urahisi, ilimradi mfanikio nyanja zote  yanawezekana kupitia mitandao ya kijamii na mfano mzuri ji mimi hapa na nitakuwa tayari kuwasaidia woote amba wanahitaji kusaidiwa kutumia vyema mitandao kupata mafanikio. 

Namalizia makala hii nikiwa bado ninayo Mazuri ambayo Raiffa  MC Golden Voice, ameyavuna kupitia mitandao ya kijmii lakini Huenda Mpendwa msomaji ukakosa ladha ya simulizi hii endapo itakuwa refu kupitiliza matarajio ni kuona  Vijana wengine wanaiga mfano huu mzuri wa matumizi ya mitandao ya kijamii kuweza kujipatia Mafanikio. 

 MWISHO. 





Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI