WANANCHI ZANZIBAR WAPONGEZA UONGOZI WA DK SAMIA.
NA MWANDISHI WETU, UNGUJA.
WANANCHI wa Zanzibar wamesema,Tanzania wamepata kiongozi ambae Taifa likimuenzi wataweza kuendelea kupiga hatua mbalimbali za kimaendeleo na hatua bora zaidi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati mbalimbali, wananchi hao wamesema, uongozi wa Dk. Samia umekuwa ukiwashirikisha wananchi wote ambapo ni sifa pekee ya kiongozi aliyekuwa bora na anapaswa kuenziwa na taifa.
Mmoja ya wananchi hao, ambae ni mzee wa maskani ya kachorora, Mohamed Mussa Seif (mkobani) alisema, endapo kiongozi huyo akiendelea kupewa ushirikiano maendeleo zaidi yatapatikana kwa wananchi ikiwemo kuwanufaisha mmoja mmoja.
Alisema, Dk. Samia, amekuwa akitambua changamoto mbalimbali za wananchi kwani uongozi wake umetokea chini na alikuwa bega kwa bega na watu na ni mpenda maendeleo na hana ubaguzi wa dini, chama wala rangi ya mtu.
Hivyo, alisema utendaji wa kazi wa Rais. Dk Samia hauna shaka kwani ni kiongozi mzoefu na mwanamapinduzi wa kweli na mpenda haki kwa watu wote na kwa rika mbalimbali ikiwemo vijana, wazee na wanawake.
Sambamba na hayo, alisema kwa kiongozi mwenye kuleta maendeleo hakukosi kutokezea watu wakakosoa ili asifanikiwe, hivyo, alisema kupitia maskani yao wataendelea kushirikiana nae kwa pamoja ili kuona maendeleo ya taifa yanafikiwa Tanzania na Zanzibar.
"Mama Samia amekuwa akifanya shughuli zake kwa ufanisi wa hali ya juu na uaminifu na hana shaka na hapendi makuu" alisema.
Nae, Ali Othman Mohamed ( Ali Beta) alisema, utendaji wa Rais Samia ni mzuri na wa kupigiwa mfano na wa kupongezwa.
Alisema, watendelea kumshika mkono na kumuombea kwa mungu juu ya uongozi wake hasa katika kuendeleza amani ya nchi kuendelea kutawala kwani wazee wameacha amani na utulivu na wananchi hawana budi kulinda amani hiyo iliyopo.
Hivyo ni vyema wananchi kuendelea kumuunga mkono dk Samia ili maendeleo yaendelee kupatikana katika taifa.
Comments
Post a Comment