WKAGUZI WA SHEHIA WAKUMBUSHWA WAJIBU WAO KWA JAMII

NA OMAR HASSANZANZIBAR                              07/08/2023

KAMISHNA wa Polisi Zanzibar  HAMAD KHAMIS HAMAD amesema uwajibikaji na utoaji wa haki kwa Wakaguzi wa Shehia kutaleta mabadiliko na kuunda jamii salama, imara na yenye mshikamano.

Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Shehia wa Mikoa mitatu ya Unguja huko Kambi ya Polisi Ziwani ameeleza kuwa uwepo wa Wakaguzi wa Shehia kunatoa matumaini kutatua matatizo ya jamii, kuzuwia na kupunguza uhalifu, kuimarisha uwajibikaji wa Polisi na kupunguza hofu ya uhalifu.

Mratibu wa Mafunzo hayo Mrakibu wa Polisi Dkt. EZEKIEL KYOGO kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Polisi Dodoma amesema mafunzo hayo yatawajenga uwezo Wakaguzi hao wa Shehia kuelewa vizuri Falsafa ya Polisi jamii na kuwa na uwezo wa kuifanyia kazi kwa ufanisi.

Kwa upande wake VERONICA FUBILE kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP amesema shirika hilo linasaidia kufanya Mafunzo hayo ni kutoa mashirikiano ya kiusalama ili kukuza Maendeleo ya Nchi.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.