KIJANA OMAR ALIEBADILI MUELEKEO KUTOKA KUWA DEREVA WA GARI HADI MKULIMA WA MBOGA MBOGA NA MATUNDA AELEZA SABABAU ZILIZOMSHAWISHI KUFANYA HHIVYO MAAFANIKIO NI MOJA KAATI YA SABABU HIZO.
NA, AMINA AHMED MOH’D - PEMBA. 0776859184
KUPITIA Siku ya Wakulima Duniani Leo Maalum Tumekuandalia Simulizi Fupi inayomuhusu Omar Salum Mbarouk Mkaazi wa Vitongoji Chake Chake Kijana Alieamua Kuacha Gari na Kushika Jembe kuzifata Fursa Zinazopatikana kupitia Kilimo na Kupata Mafanikio.
Kijana Huyo Ambae Kwa Zaidi ya Miaka 4 Alikuwa Anajishughulisha na Udereva Wa Gari ndogo Za kubebea Mizigo Amesema kuwa katika Kipindi chote hicho Hakuna Mafanikio ya kujivunia Ambayo ameyapata kupitia Shughuli ua Udereva.
Ni kipindi cha Muda Mfupi Tangia Omar kuanza Rasmi shuguli za Kilimo Cha Matunda na Mboga mboga Vitongoji ambapo Kwa Sasa Ameamua Rasmi Kuwekeza nguvu Zake zote katika shuguli za Kilimo.
Miongoni mwa Kilimoambacho Anaendelea kulima Omar ni Pamoja Migomba, Pilipili, Matikiti, Mahindi, mipensheni pamoja na Ufugaji wa Kuku.
Omar Salum Mbarouk - Mkulima.
Anasema Mvuno wa kwanza wa Zao la Matikiti Alisema Tayari Zimempatia Matunda kwani Tayari Amenunua Matofali Pamoja na mawe kwajili ya kuanza shughuli za Ujenzi wa nyumba Yake.
Kilimo kikiwa kinaendelea kwa kijana Omar anasema Matarajio ya mafanikio ni makubwa baada ya Mavuno kuputia zao la Migomba kukamilika.
Anasema Ndizi ni Miongoni mwa Biashara yenye uhitaji mkubwa katika soko la Ndani ya Kisiwa cha Pemba lakini hata nje ya kisiwa Hicho.
"Msimu wa mavuno ya Ndizi utakapowadia Ninamatarajio makubwa kujipatia kipato cha kuendesha harakati hizi za kilimo lakini Pia kuendeleza shughuli za Ujenzi".
Omar amabe Amehamisha Makaazi yake na kuamua Kupiga kambi nje kidogo na Kijijini kwao Kufanya shughuli hizo za Kilimo kwa Ufanisi Anasema Licha ya kulima Kilimo hicho lakini Pia Ufugaji wa kuku wa kienyeji Umeanza kuimarika kutoka kuku 5 Aluokuwa nao kabla hadi kufikia 20 ambao wote hao wanaendelea na uzakishaji wa vifaranga ambavyo muda mfupi baadae vitaweza kuwa Tija kwa uoande wake.
Aliemshawishi Omar kujiunga na Kilimo ni Mama yake Mzazi Ambae kwa Muda mrefu anafanya shuvhuli hizo.
"Nilihamasika kupitia Mama yangu Mzazi bi Mkunga anapata fursa mbali mbali kuputia kilimo, Hamasa ilizidi baada ya kuona Amenunua mbuzi wawili 2 kama faida licha ya vitu vyengine mbali mbali zilizitokana na kilimo.
Napata Mafunzo mbali mbali knamna na mbinu bora za kilimo kutoka kwa mama yangu ambae nae alichowezeshwa na MRADI WA VIUNGO unaotekelezwa na TAMWA-Zanzibar kwa mashirikiano kati ya , PDF, CFP kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya EU kupitia Mpango wa Agri conect. "
Omar amewataka Vijana wenzake Kutopuuza Fursa za kilimo na badala yake kujikita na kuwekeza katika kilimo ili kujikomboa kimaisha.
Anasema Kilimo kinaweza kutimiza ndoto ya kijana yeyote ambae ataamua kulivalia njuga suala hilo katika kujikomboa.
Omar Pamoja na Mambo mengine hakusita Kuiomba Serikali na wadau kumtembelea katika shamba lake ili kumpatia Zaidi Elimu Ambayo itazidisha Hamasa katika kukiendeleza Kilimo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment