MFUMO WA BENKI KUTUMIKA KULIPA VIBALI VYA NGOMA ZA UTAMADUNI MASHEHA WAPEWA AGIZO.
Na AMINA AHMED Masheha wa Shehia Wa mkoa wa kusini Pemba Wametakiwa Kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kupitia utowaji wa vibali vya ngoma mbali mbali ili za utamaduni kwa kutumia mfumo wa ulipiaji wa benki na kusaidia serikali kuongeza na kukusanya mapato yake bila kupotea . Akizungumza katika mkutano maalum na masheha mkoa wa kusini Pemba Katibu Mtendaji baraza la sanaa sensa filamu na utamaduni Zanzibar Dk Omar Abdalla Adam Amesema iwapo vibali hivyo vitatolewa kupitia mfumo huo wa ulipiaji ambao ni mfumo mpya wa kidigitali fedha zinazotolewa zitasaidia kutumika katika kupanga mambo mbali mbali ya serikali ambayo yatasaidia kuleta maendeleo kwa Wananchi. Dk OMAR ABDALLA ADAM KATIBU MTENDAJI BARAZA L BARAZA LA SANAA SENSA SENSA NA UTAMADUNI ZANZIBAR. Aidha Katibu Adam amewataka Masheha hao kuendela kuhifadhi mila silka na tamaduni za kizanziba...