JESHI LA POLISI ZANZIBAR LATOA NENO Hili.


Na AMINA AHMED. 

Nawaombea aibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya jinai wa jeshi la Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Zubeiri Seif Chembera amesema mashirikiano makubwa wanayoyapata kutoka kwa viongozi wa ngazi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi kumerahisisha kazi za kuzuia matendo ya uhalifu na maskosa ya jinai kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
 
ACP Chembera ameyasema hao huko Makao Makuu ya jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ziara yake ya siku tatu ya ukaguzi na kuagalia utendaji kazi wa jeshi hilo katika mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba na kueleza kuridhishwa kwake na uwajibika wa askari wa jeshi hilo katika ngazi mbali mbali.
 
Amesema Jeshi la Polisi Zanzibar litaendelea kushirikiana na viongozi hao ikiwemo kuifanyia kazi michango yao mbali mbali wanayoitoa katika kuboresha kazi zao za kuweza kupambana na vitendo vya uhalifu na makosa mbali mbali katika jamii.
 
Aidha ACP Chembera amewataka wananchi kutoa taarifa Za kiuhalifu ikiwemo madawa katika vituo vya polisi vilivyopo karibu nao sambamba na kuacha muhali katika kutoa ushahidi wa kesi mbali mbali zinazopelekwa mahakamani na jeshi hilo.
 
Katika hatua nyengine Kamishna huyo amewataka wananchi kutokujichukulia hatua mikononi pale wanamkamata watuhumiwa wa makosa mbali mbali ikiwemo ya wizi wa mifugo na mazao na wawafikishe kwenye vyombo vya sheria.
 
Katika ziara hiyo ya siku tatu kisiwan Pemba Naibu Kamishna amekutana na kuzungumza na wakuu wa wilaya,masheha, kutembelea mahabusu, sambamba na kukagua utimamu wa askari katika kupeleleza na kusimamia kesi pamoja na kusikiliza changamoto za askari wa kitengo cha upelelezi katika mikoa hiyo miwili.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI