MSAADA WA CHAKULA WAWANUIFAISHA WANANCHI WENYE HALI DUNI KISIWANI PEMBA.
Na Fatma Abrahman.
Mkuu wa mkoa WA kusini Pemba Matar Zahor masoud Ameipongeza taasisi the future life foundation katika hatua wanazozichukua za kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum pamoja na kuwafariji kwa kuwapatia mahijaji muhimu Ili nao kuishi kwa amani .
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huyo mkuu wa wilya ya chake chake Abdalah Rashid Ali amesema kuwa kujitoa katika kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum ni jambo jema hivyo ni vyema kuniwekea hakiba ya baadae.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya ugawaji wa msaada huo raisi wa taasisi ya the future life foundation sheikh Mbarouk Seif Salim amesema wametoa sadaka hio kwa mayatima wasiopungua 320 ambapo lengo ni kutoa zaidi ya kiwango hicho Ili kuwasaidia na kuwafanya wajione kua nao ni sawa na walio na wazazi licha ya kuondokewa na wazazi wao .
Kwa upande wa wa wazazi na walezi wa mayatima hao wameishukuru Jumuiya hio na kuyaomba mashirika mengine kuiga mafano wa Jumuiya ya the future life foundation kwani ni kutoa ni kujiwekea hakiba ya baadae .
Msaada huo wa Michele umetolewa na taasisi ya the future life foundation kisiwani Pemba chini ya ufadhili wa kutoka Nchini Canada , ufaransa pamoja na Ubeligiji
Comments
Post a Comment