UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA UWT WILAYA YA CHAKE CHAKE WAPATA VIONGOZI WAPYA.
Na AMINA AHMED
Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Chake Chake Mkoa kusini Pemba umefanya uchaguzi ambapo umemchagua Bi Halima Juma Khamis Kuwa mwenyekiti mpya atakaeongoza umoja huo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi huo mafunda Hamad Rubea amewataka waliochaguliwa kufanya kazi kwa uadilifu kutumikia jumuia hiyo.
Awali Wakizungumza na Habari hizi baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu Umoja wa wanawake wilaya hiyo Akiwemo Zuhura Mgeni othman , Aziza Yussuf Salum pamoja na Mwajuma Hija kipenda wamesema Uchaguzi huo utasaidisa kuleta maendeleo kwa wanawake wa umoja huo katika kutetea maslahi mbali mbali katika ngazi za juu za Chama huku wakiwataka watakaochaguliwa kutumikia kwa uadilifu nafasi walizoziomba.
Uchaguzi wa kupata viongozi watakaoongoza umoja huo wilaya ya Chake Chake umefanyika Leo katika ukumbi wa makonyo Wawi.
Ambapo jumla ya nafasi Sita zilpigiwa kura ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania UWT wilaya Chake Chake, Mjumbe mmoja wa UWT halamashauri kuu CCM wilaya ya Chake Chake, Wajumbe 8 baraza umoja wa wanawake wilaya ya Chake Chake, Mjumbe mmoja mkutano mkuu taifa wilaya ya Chake Chake, Mjumbe 1 wa kuwakilisha jumuia ya wazazi UWT wilaya ya Chake, pamoja na Mjumbe mmoja kuwakikisha vijana UWT wilaya ya Chake Chake.
Comments
Post a Comment