MFUMO WA BENKI KUTUMIKA KULIPA VIBALI VYA NGOMA ZA UTAMADUNI MASHEHA WAPEWA AGIZO.
Na AMINA AHMED
Masheha wa Shehia Wa mkoa wa kusini Pemba Wametakiwa Kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kupitia utowaji wa vibali vya ngoma mbali mbali ili za utamaduni kwa kutumia mfumo wa ulipiaji wa benki na kusaidia serikali kuongeza na kukusanya mapato yake bila kupotea.
Akizungumza katika mkutano maalum na masheha mkoa wa kusini Pemba Katibu Mtendaji baraza la sanaa sensa filamu na utamaduni Zanzibar Dk Omar Abdalla Adam Amesema iwapo vibali hivyo vitatolewa kupitia mfumo huo wa ulipiaji ambao ni mfumo mpya wa kidigitali fedha zinazotolewa zitasaidia kutumika katika kupanga mambo mbali mbali ya serikali ambayo yatasaidia kuleta maendeleo kwa Wananchi.
Dk OMAR ABDALLA ADAM
KATIBU MTENDAJI BARAZA L BARAZA LA SANAA SENSA SENSA NA UTAMADUNI
ZANZIBAR.
Aidha Katibu Adam amewataka Masheha hao kuendela kuhifadhi mila silka na tamaduni za kizanzibari ili vizazi vya sasa na baadae viendeleze kurithi tamaduni zao.
Aliwataka masheha hao pia kuendela kutatua na kusimamia kero mbali mbali zinazojitokeza katika jamii katika kuona utamaduni haupotezi asili yake katika jamii.
Kwa upande wake Ofisa Mdhamini wizara ya Habari Vijana utamaduni na michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau amewataka masheha hao kubadilika kuendana na wakati katika kutumia mfumo huo ambao unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa 11 mwaka huu kwa kuhifadhi risiti hizo ili kuepuka kuingia hatiani endapo zitahitajika serikalini.
Mfamau Lali Mfamau
Ofisa Mdhamini WHVUM Pemba.
Wakizungumza Baadhi ya masheha hao akiwemo Safia Khamis Hamad, shehia ya shamiani mwambe na Muhammed Nassor Khamis shehia ya kilindi wameiomba wizara ya Habari kupitia baraza la sanaa kusaidia kutoabelimu hiyo ya mabadiliko ya ulipajibwa vibali kwa wananchi ili kuepuka usumbufu wa kutokupingwa kwa agizo hilo.
Aidha baadhi ya masheha hao akiwemo Haji Ali Shaame kutoka shehia ya kisiwa Panza Massoud Muhammed Shehi ya wara pamoja na Ali khamis Massoud wameliomba baraza hilo kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo za kibenki katik maeneo yao ikiwa ni pamoja na huduma za wakala wa Pbz ili kuwaepushia usumbufu wananchi watakapo fikisha agizo hilo.
Mfumo huo mpya wa ulipaji wa vibali vya ngoma kupitia benki unatarajiwa kuanza rasmi October 1 ambapo elimu hiyo imetolewa leo kwa masheha wa kusini Pemba.
mwisho
Comments
Post a Comment