DC Mjaja afungua kongamano la Amani lililoandaliwa na Taasisi ya Roots & Shoots kwa wanafunzi

 


Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja amesema maendeleo yakiwemo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika taifa lolote hutegemea kuwepo na kuimarika amani, umoja na mshikamano.

Amesema wajibu kwa wananchi wote bila ya kujali dini, rangi, kabila na tofauti zao katika mitazamo ya kisiasa hivyo kila mmoja anao umuhimu wake katika kujenga misingi imara ya amani.

Mjaja ameyasema hao huko katika Skuli ya Sekondari ya Moh`d Juma Pindua Mkanyageni Wilaya ya Mkoani wakati akifungua kongamano la umuhimu wa amani lililoandaliwa na Taasisi ya Roots & Shoots kwa wanafunzi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya amani duniani.

 Aidha mjaja ameipongeza taasisi ya Roots & Shoots kwa shughuli zao mbali mbali wanazozifanya katika jamii ikiwemo kuwajenga wanafunzi kuwa wabunifu.

Akizungumza kwenye Kongamano hilo Mratibu wa Roots & Shoots Mkoa wa Kusini Pemba Matti Ali Matti ameeleza umehimu wa kuwepo wa amani, umoja na mshikamano.

Akisoma risala kwa niaba ya Taasisi hiyo Hussein Abdalla Bakar amesema kufuatia dunia kupotenza misingi yake ya amani ni vyema kuitumia siku hii kuamsha ufahamu juu ya athari za kutokuwepo kwa amani.

Maadhimisho ya siku ya Amani duniani huanzimishwa kila ifikapo tarehe 21 septemba ya kila mwaka na haya ni maadhimisho ya 21 tokea kupitishwa azimio la siku ya amani duniani na umoja wa mataifa.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI