WAANDISHI WASUKWA UANDISHI WA HABARI ZA MAENDELEO KWENYE JAMII

 

Habari zenye kuleta mabadiliko katika jamii ni chachu ya maendeleo  nchini kuhamasisha wanawake kutumia haki ya kidemokrasia na uongozi hali itakayosaidia kushiriki na kushinda kwenye ngazi za maamuzi.

 Akizungumza na waandishi wa habari vijana Zanzibar  mkufunzi kutoka Chama cha wandishi wahabri wanawake Tanzania (TAMWA) Dr. Ananileya Nkya amesema ili kufikia maendeleo ya wanawake nchini na kupata mwamko wa kushika nafasi za uongozi ni vyema waandishi kubadilika katika uandaaji wa kazi zao .

 Ameongeza kuwa waandishi waliowengi huandika habari za kuibua changamoto tu jambo linalopelekea kuchelewakwa maende;leo katika jamii .

 Shifaaa Said Hassan kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) ofisi ya Zanzibar   amewaasa waandishi kutumia fursa ya mafunzo katika kuandaa maudhui ya kihabari kupitia kalamu zao.

kwa upande wao shiriki wa mafunzo hayo, Ahmed Iddi Haji na Esau Simon Kalukubila wamesema mafunzo hayo yatasaidia kuandika habari zenye kuleta mabadiliko ndani ya jamii na tasnia ya habari.

Mkutano huo wa siku tatu ni muendelezo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandshi wa habari vijana katika kuandika habari za suluhisho kupitia  mradi unaosimamiwa na TAMWA Zanzibar Kwa ufadhili wa National Endowment for Democracy nchini Marekani.

 

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI