JUMUIA YA WAZAZI CHAMA CHA MAPINDUZI YAASWA KUWA WABUNIFU.
Na AMINA AHMED.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Chake Chake Hassan Khatib Hassan amewasa viongozi Wlwatakaochaguliwa kungoza Jumuia ya wazazi kuwa wabunifu kubuni miradi ya maendeleo itakayosaidia kuendesha Jumuia hiyo mbele kimaendeleo .
Katibu Hassan Aliyasema hayo Alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Chake Chake katika ghafla ya uchaguzi wa Jumuia hiyo uliofanyik katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake.
Alisema Iwapo viongozi hao watakuwa wabunifu katika Suala la miradi ya maendeleo Chama kitaendelea kuwaunga mkono katika kufikisha mbali kimaendeleo Jumuia hiyo .
Aidha alisema kuwa matarajio ya viongozi watakaopata nafasi ya kuongoza Jumuia hiyo kwa miaka mitano katika nafasi mbali mbali ni kusimamia Jumuia hiyo na kuona Inafika mbali katika ushindani wa vyama vingi mwaka 2025.
Awali kwa upande wake Katibu wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Chake Chake kupitia Chama Cha Mapinduzi Fatma Ramadhan Khamis Aliwaasa wajumbe wa mkutano mkuu Jumuia ya wazazi wilaya ya Chake Chake kutoa mashirikiano kwa viongozi watakaoteuliwa kuongoza Jumuia hiyo ili kuzidisha uimara katika Chama na Jumuia hiyo ambayo ni Jumuia mama kwa Chama hicho.
Fatma Ramadhan Khamis.
Katibu Jumuia ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Chake Chake.
Wakizungumza baadhi ya wajumbe wa Jumuia ya wazazi akiwemo Hadija Henoc pamoja na Khamis Ali khamis wamewaomba viongozi hao Kusaidia kuongeza wananchama katika Jumuia hiyo pamoja kuimarisha utendaji katika Jumuia na Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuwezesha sambamba na kuondosha makundi ambayo ya nakuwa yanajitokeza katika kipindi Cha uchaguzi .
Hadija Henock Mjumbe Jumuia ya wazazi Chake Chake.
Jumuia hiyo umefanya uchaguzi wa nafasi mbali mbali ambapo viongozi watakaoteuliwa wataongoza Jumuia hiyo kwa kipindi Cha miaka mitano IJAYO.
Mwisho
Comments
Post a Comment