WAHAMASISHAJI JAMII WAPEWA MAFUNZO PEMBA
Na Fatma Suleiman
Wahamasishaji jamii kisiwani Pemba wametakiwa kutumia fursa ya mafunzo ya uongozi waliyopatiwa Ili kusaidia wanawake kushiriki kwenye demokrasia siasa na uongozi.
Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Afisi ya mrajisi asasi zisizo za kiserekali Pemba Sada Abubakar Khamis wakati akifungua mafunzo ya siku mbili Kwa wahamasishaji jamii, watu wa dini na watu wenye ulemavu.
Aidha ameongeza kuwa serekali ya muungano wa Tanzania na serekali ya mapinduzi ya Zanzibar zimetoa vipaumbele kwa mwanamke kushika nafasi mbali mbali hivyo ni wajibu wao kuzichangamkia fursa hizi katika kusonga mbele.
Alizungumza afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka chama Cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa _ Zanzibar amesema kupitia mradi huu wanatarajia kufikia watu million Moja na laki Tano wanawake wakiwa zaidi ya elfu kumi na Tano, wanaume elfu kumi na sita, waandishi wahabari mia mbili, wasichana kutoka vyuo vikuu na skuli mia sita, wanaasasi za kiraiya mia Moja hamsini.
Hafidh Abdi Said mkurugrnzi PEGAO
amesema mbali na juhudi zinazochukuliwa ila Bado ushiriki wa wanawake ni ndogo hivyo, ni vyema kushirikiana kwa pamoja kuhamasisha Ili wanawake kufaidika na kujitoa kushika nafasi za Uongozi ambapo ndio lengo la mradi.
Akiwasilisha mada ya demokrasia mkufunzi wa mafunzo hayo ambae pia ni mwanaharakati Fat_hiya Mussa Said amesema muda umefika kwa wanawake kutumia haki Yao kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa kama Katiba inavyoelekeza bila ya kubugudhiwa.
Wakitoa maoni yao baadhi ya wahasishaji jamii
Comments
Post a Comment