RASIMU YMPYA YA SERA YA HABARI MBIONI KUKAMILIKA.
WIZARA ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, imesema ipo hatua nzuri ya kukamilisha rasimu mpya ya Sera ya Habari Zanzibar inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya Habari nchini.
Waziri wa Wizara hiyo Tabia Maulidi Mwita alieleza hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mafanikio katika wizara hiyo ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais mwinyi madarakani huko katika ukumbi wa ZBC Mnazi Mmoja.
Alisema Sera hiyo inatokana na marekebisho katika Sera ya Habari ya mwaka 2005 imechukua muda kukamilika kutokana na kupitia marekebisho ya mara kwa mara yanayotokana na maoni ya wataalamu wa kisheria na wadau wa kada hiyo nchini.
Alisema Kwa sasa Sera hiyo inatarajiwa kupelekwa katika taasisi mbali mbali zinazosimamia habari nchini ikiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT) ili kutoa mapendekezo na baadae kupelekwa barazani na kupitishwa.
Hivyo aliwataka wadau wa Habari nchini kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki cha kukamilisha mchakato huo.
Akizungumzia sekta ya Michezo nchini Waziri Tabia alisema serikali imefanikiwa kuanza kwa maboresho ya Miundombinu ya viwanja vya Michezo Zanzibar awamu ya pili ikiwemo uwanja wa Amani na Gombani Pemba ili kukidhi Vigezo vya CAF na FIFA katika michuano ya mataifa ya Afrika Kwa wachezaji wa ndani maarufu CHAN Inayotarajiwa kuanza mwezi February 2025.
Hata hivyo amegusia mpango wa ujenzi wa uwanja mpya wa Michezo unaotarajiwa kuchukuwa watazamaji 35000 ili kutumika katika michuano ya AFCON 2027.
Comments
Post a Comment