KUNA MABADILIKO MAKUBWA YA ONGEZEKO LA UKUSANYAJI MAPATO KIPINDI CHA MIAKA 4 YA DK MWINYI

  Mapato Zanzibar,ZRA imesema ongezeko la ukusanyaji wa mapato umekuwa ukiimarika kila mwaka tokea kuangia madarakani kwa Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi mwaka 2020.
Akitoa taarifa ya makusanya kwa kipindi cha miaka 4 ya Rais Dkt. Mwinyi kwa waandishi wa habari huko Ofisi Kuu ya ZRA Pemba, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar Said Ali Moh`d amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kuimarishwa kwa miundombinu ya kiuchumi nchini.
Kaimu Kamishna Mkuu huyo amesema katika mwezi wa Oktoba mwaka huu ZRA idikadiriwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 74.549 lakini wamevunga lenga kwa kufanikiwa kukusanya jumla ya Sh bilioni 76.528 ikiwa ni sawa asilimia 102.65.
Amesema makusanyo hayo ni ongezeko la bilioni bilioni 15.326 ukilingalisha na makusanyo ya mwezi kama huu wa Oktaba katika  mwaka 2023 ambapo amesema makusanyo hayo yamechangiwa na usimamizi na miongozo kutoka kwa Viongozi wao chini ya Rais Dk Husein Ali Mwinyi na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Sada Mkuya.
‘’Mamlaka ya Mapato katika Mwezi wa Oktoba mwaka huu tumefanikiwa kukusanya Bilioni   76.528 ikiwa mamlaka hiyo ilikadiriwa kukusanya bilioni 74.549 ikiwa ni ongezeko la asilimia 102.65 alisema.
Aidha amesema kuwa katika katika kipindi cha mwaka wa fedha Julai - Oktoba 2024/25 Mamlaka imeongeza makusanyo ya serikali kwa kila mwezi kwa kukusanya jumla ya bilioni 277.46 ikiwa ni sawa na bilioni 69.365 ukilinganisha na  mwisho wa mwaka wa fedha wa 2023/24 ambapo waliweza kukusanya wastani wa shilingi bilioni 59.90 kwa mwezi.
Kwa upande wake Mkurugenzi  wa ZRA  Pemba,Jamal Hassan Jamal amewashukuru wananchi wa Zanzibar hasa Pemba  kwa kuendelea kutoa mashirikiano kwa Mamlaka hiyo katika kazi yake ya ukusanyaji wa Mapato ya Serikali na kuendelea kuwasisitiza kushirikiana zaidi kwa kudai risiti za kielektroniki kila wanapofanya mahitaji yao katika maduka.
‘’Tunawashukuru wananchi kwa kutupa mashirikiano katika ukusanyaji wa mapato kwa hiari kwani ndio inayotumiwa na Serikali katika kutekeleza miradi mbali mbali ya Maendeleo Nchini na nawaomba muendelee kushirikiana nasi kwa kudai risiti za kielektroni wakati mnapofanya manunuzi’’alisema Jamal.
MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.