ZCRF YATOA MAFUNZO YA SIKU 2 KWA WATETEZI WA HAKI ZA WATOTO PEMBA


Jukwaa la haki  za Watoto Zanzibar (ZCRF) ,imetoa mafunzo kwa jumuia zalinazohusiana na  watetezi wa haki za watoto Pemba   yenye lengo la  kuwajengea uwezo  wa kisheria  katika utendaji kazi wa kusimamia  haki za watoto   yaliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Madungu Sekondari leo July 6 .

Akifungua  mafunzo kwa wawakilishi wa jumuia 20 ambazo shughuli zake zinawagusa  na kuwatetea watoto zaidi  kisiwani humo Mratibu  wa jukwaa hilo Saphia Lengali  amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kusaidia watoto ambao bila utetezi  hawawezi kusimamia upatikanaji wa haki zao wenyewe .

Amesema suala la haki za watoto ni suala linalotambulikana kwa  mikataba  ya kimataifa sheria Tanzania na  Zanzibar  hivyo wajibu wa kulinda haki zao  ni suala  linalohitaji ulinzi madhubuti katika sera na sheria hizo kwa kuimarisha zaidi  ulinzi na makuzi ya mtoto.

Katika mafunzo hayo mada na maoni mbali mbali yalitolewa katoka kuboresha na kuimarisha ulinzi wa mtoto kwa mujibu wa sheria .


Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.