WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AIPA KONGOLE HOSPITALI YA KINYASINI KWA HILI
NW MWANDISHI WETU ,WIZARA YA AFYA PEMBA
WAZIRI wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amefanya ziara maalum katika Hospitali ya Wilaya Kinyasini ambayo ilikuwa na lengo la kuangalia hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi wanaofika hapo kufata huduma mbali mbali.





Ambapo taarifa ya utendaji kutoka kwa daktari hospitalini hapo juu ya mama wajawazito na watoto wanaozaliwa ni ya kuridhisha ambapo hakujawahi kutokea kifo chochote cha mama mjazito na watoto.
Sambamba na hayo Mazrui pia ametoa maelekezo kuhusu upatikanaji wa majibu ya maabara kwa wagonjwa yaweze kutolewa kwa haraka .
Comments
Post a Comment