WAUGUZI WANAWAKE WANAVYOHITAJIKA KWENYE MICHEZO ZANZIBAR.


NA ASIA MWALIM

UNAPOMUONA njiani, hudhani kuwa ni mwanamke mwenye kipaji kikubwa viwanjani.

Unaweza ukasema ni mrembo au dada aliyezoea kukaa ndani tu kufanya shughuli za urembo na kusubiri mahitaji kutoka kwa familia yake.

Hali hiyo inatokana na urembo wake aliozaliwa nao ingawa ukweli ni dada mchapa kazi na mwenye ujasiri wa hali ya juu.

Sauti yake nzuri ikiwa na ukavu kwa mbali, sio nzito wala nyepesi ambayo inafahamika kwa haraka kwa yule atakaesikiliza.

Huyo ni Rahma Abdallah Munir, (29) ambae hivi sasa anajulikana kama daktari wa kike katika timu ya Baraza la wawakilishi Zanzibar (BLW).

Rahma umaarufu wake mkubwa aliupata wakati alipochaguliwa kuwa daktari mkuu timu za wanawake Zanzibar kupitia ZFF mwaka 2020.

Ilipofiika mwaka 2018 alianza kutumikia nafasi ya udakatari (muuguzi)wa timu ya Malindi sports Club baada ya kumaliza masomo yake ya stashahada kutoka chuo cha Afya huko amachina Mwanzo (Zanzibar  School of Health).

''Niliingia kwenye Sport Injury with Medicine kuanzia timu ya Malindi Sport Club kwa mara ya kwanza lakini sikuwa na hofu ya kazi kwa sababu najiamini pia nikiwa na ari ya kufanya kazi hiyo" alisema.

Wakati huo alimaliza masomo yake akiwa kama mwanasaikolojia kutoka Zchuoni hapo alifanya kazi hiyo hadi mwaka 2019.

Ilipofika mwaka 2020 alichaguliwa katibu wa madakatari ZFF ambapo ilipofika mwaka 2022 alipata nafasi ya kushiriki kama daktari wa baraza la wawakilishi hadi sasa.

"Najivunia kuwa mwanamke anaewajibika kwenye eneo hilo bila hofu nashiriki katika mazinga yote nahudumia wanawake na wanaume, daktari hachagui nani wa kumtibu akiwa mwanamke au mwanamme" alisema.

Alisema madaktari viwanjani wapo kwa ajili ya kuona afya za wachezaji zinatengemaa ili waendelee na zoezi mpaka mwisho wa mchezo.

Rahma anajivunia kuwa mwanamke anaehimili kufanya kazi katika mazingira magumu.

Alisema jambo kubwa linalompa ari ya kuafanya kazi ni kuipenda kazi hiyo na mahala popote na unaweza kufanya kazi.

Kila penye mafanikio hapa kosi changamoto kwa upande wa Rahma changamoto kubwa inayomsumbua ni ile ya kutakiwa kimapenzi na baadhi ya wachezaji anaowapatia huduma.

"kwangu mimi jambo hilo sikulipa uzito mkubwa kwa sababu kila mahala changamoto hii ipo na uhalisia unaonesha kuwa panapokuwa na jinsia za watu tofauti mambo kama haya yanweza kutokea kwa asilimia kubwa" alisema.

Mwanamme anapotaka kufanya ushswishi kwa mwanamke hufanya mahala popote haijalishi yupo katika mazingira gani hata kwenye vita yupo tayari kumshawiwshi mwanamke kimapenzi.

Alieleza kuwa wakati anaanza na harakati za kujishughulisha na udaktari kwenye timu za mpira alipata ugumu kiasi fulani kiasi kwamba wapo waliwahi kumkatisha tamaa kwa vitendo na maneno.

"Kwangu mimi maneno hayakuniathiri kwani nilizidisha juhudi zangu kusimamia malengo yangu yaweze kutimia" alisema.

Alisema familia nyingi zinawafanya watoto wa kike kana kwamba hawawezi kufanya kazi mazingira ya timu za mpira au sehemu nyengine za michezo jambo ambalo linawanyima fursa wanawake.

Rahma alikiri kuwa wanawake wengi amewashuhudia hawawezi kufanya kazi sehemu ambazo yeye amefanya na anaendelea kufanya kutokana na imani potofu walizobeba kutoka kwa jamii.

Jamii kubwa wanadhani mtu akiwa daktari lazima afanye kazi hospitali, au vituo vya afya kumbe kuna mazingira mengi ambayo mtu anatikwa kufanya kazi ikiwemo kwenye timu za mpira.

Akizungumzia mashirikiano yake na familia alisema hajawahi kukatishwa tamaa na familia yake inamuunga mkono kwa jambo hilo ambalo ni ndoto yake.

"familia yangu ipo pamoja na mimi kwa kila hali, haijawahi kunigeuka wala kuniacha mkono kwenye kazi zangu"alisema.

Katika familia yake hakuna mchezi ndani wa kike, ingawa mama yake mzazi alikua mpenzi wa mpira kwa kutizama na kufatilia timu mbali mbali ikiwemo Simba na Yanga.

Rahma anasema kuna haja ya kuwepo madaktari wengi wanawake hapa Zanzibar kwani timu zipo nyingi lakini wauguzi wanaume wanaonekana wengi kuliko wanawake.

Jambo hilo litahamisisha watoto wa kike kushirki michezo sambamba na kushajihisha madaktari wanawake kufanya kazi maeneo kama hayo.

Rahma aliwataka wachezaji kupokea madakatiri wanawake kama walivyo madaktari wakiume, wasiwavunjie heshima au kuvuka mipaka kwa kuangalia jinsia zao.

"Sisi tunapokwenda viwanjani kwa sasbu ya kazi maalumu watuchukulie tupo kwenye kazi na sio vyenginevyo" alisema.

Alisema ili idadi ya madaktari wanawake iongezeke kwenye timu ni lazima jamii iondoshe dhana ya kuwa wanawake wanafanya kazi kwenye vituo vya afya pekee yake badala yake kujitokeza kwenye maeneo hayo.

Jambo jengine ni madaktari wa kiume kutoa mashirikiano kwa madakati wanawake hasa wanapokua wapya kwenye viwanja.

"Mara nyingi daktari mwanamke kama hujazoea huwezi kwenda kiwanjani peke yako mpaka upate msaidizi hasa wa kiume ili kukuongoza kwani baadhi ya wachezaji wakorofi kwa mtu wasiye mjua" alisema.

Aliomba serikali na wadau wa michezo kuwapa nafasi madakati wanawake kwani wana uwezo wa kufanya kazi hizo bila ya kuvunja sheria na mipaka.

"Sisi tupo kwa ajili ya kutibu wachezaji hatuangalii jinsia zao, tunafanya juhudi kuhakikisha mchezaji anakuwa sawa" alisema.

Miongoni mwa mafanikio ya Rahma ni kupata cheti cha daktari bora wa vilabu 16 vya Zanzibar, timu yake iliwakilisha ubingwa wa FA mwaka 2018/ 2019 kwenye kombe la shirikisho pia amefanikiwa kupokea zawadi kadhaa ikiwemo vyeti, medali, na pesa taslim sambamba na kusafiri nchi mbalimbali ikiwemo misri.

WACHEZAJI

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Zimamoto wamesema huduma wanzotoa madaktari/ wauguzi wanawake ni nzuri kwani mara nyingi wanafanya kazi wakiwa na huruma.

wanawake mara nyingi wanapotoa huduma kwa wachezaji zinapendwa kwani huonesha kujali zaidi na kutoa faraja kwa wachezaji.
 
VYAMA VYA MICHEZO ZANZIBAR.
Mrajisi wa Vyma Vya Michezo Zanzibar Abubakar Muhammed Lunda, alisema bado Zanzibar kuna wauguzi wanawake kidogo jambo ambalo linarudisha jitihada za watoto wa kike kushiriki michezo.

Aidha alisema matarajio yao kupata Madaktari wanawake wengi katika siku zijazo kutokana na elimu inayotolewa kwa jamii mara kwa mara.

"Wakati huu tunapokua viwanjani tunawashuhudia wanawake kuongezeka ijapokuwa wanakuja kuangalia tu lakini wamehamasika ukilinganisha na miaka ya nyuma" alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga viwanja vikubwa na vya kisasa kwenye maeneo mbali mbali vitahamasisha ushiriki wa wanawake ikiwemo madakatari kukimbilia kwenye timu.
Katibu wa Chama Cha Soka wilaya ya Mjini, (UDFA) Mohammed Rashid Bwaksi, alisema ni vyema jamii kuhamasisha wanawake kukimbilia nafasi hizo kwani wauguzi waanawake bado wachache.

kuwepo kwa wauguzi wanawake kwenye timu za michezo kutaleta maendeelo mengi ikiwemo kuwahamaisha watoto wa kike kushiriki michezo kwani watapatiwa huduma na wanawake wenzao.

"Pale mtoto wa kike akipata Injury na ametibiwa na mwanamke mwenziwe atajisikia faraja yeye na watu wake wa karibu hasa familia yake" alisema.

Baadhi ya wazazi wanawakataza watoto wao lkushiriki michwzo kwa madai ya kuwa kwenye timu za mpira kuna tabia chafu na muingiliano mkubwa na wanaume hivyo kukiwa na madaktari wanawake itahamasisha wazazi kupata moyo wa kuwaruhsu watoto wao.
 
WADAU WA MICHEZO
Hija Ramadhan, Mshauri masuala ya Michezo kutoka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Ujerumani (GIZ) alisema bado kuna pengo kubwa kwa wanawake kwenye michezo kuanzia wachezaji na maeneo mengine kama wauguzi.

Aliongeza kuwa jitihada za kutengeneza usawa wa kijinsia ni pamoja na kuhakikisha waadau wanashirikiana kuwalinda watoto na wanawake dhidi ya ukatili, hivyo madaktari wanawake hawapaswi kuwa na hofu ya kwenda viwanjani.

"Lengo hili tunaweza kulifikia kwa kutumia mbinu tofauti ikiwemo Michezo kwa Maendeleo," alisema Ramadhan.

Khairat Haji, Afisa Programu wa Michezo kutoka Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania, TAMWA -ZNZ, alisema bado zanzibar kuna idadi ndogo ya wanawake wanaojihusisha na masuala ya michezo.

Kwa ujumla alieza jitihada kubwa inahitajika ili eneo la michezo kutumiwa ipasavyo ikiwemo kushiriki na kushirikishwa katika kupata wachezaji hata waamuzi.

Alisema TAMWA kwa kushirikaina na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Ujerumani (GIZ) imeamua kuja na mradi huo ambao umekusudia kuboresha sekta ya michezo kwa wote nchini.

Mkurugenzi waChama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA ZNZ, Dk. Mzuri Issa alisema ni vyema wanawake kupata nafasi za kuongoza kwenye michezo kwani jamii bado ina mitazamo potofu juu suala hilo.

Alisema watoto wakike wanapaswa kupata matumaini kwa kupewa fursa ili nao kwenda mbele kwenye michezo kupata maendeleo ya kifedha, mwili na maendeleo kiujumla.

Alisema jamii imetoka mbali kwenye masuala ya kijinsia na maeneo mengi wanawake waliachwa nyuma katika muda mrefu uliopita ikiwemo mchezo.

Alisema kuna pengo kubwa la wanawake kukosa fursa za michezo hivyo kukosa matunda ya nchi.

DK.Mzuri alisema licha ya michezo kuimarisha afya lakini pia inachangamsha akili kupata kukumbuka vizuri, kuengeza kipato na kupata mawasiliano na watu mbali mbali. 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.