WAAMUZI WANAWAKE NI KIDOGO ZANZIBAR
NA ASIA MWALIM
SOKA la wanawake linazidi kukua kutokana na kuongezeka timu za jinsia, ingawa kuna idadi ndogo ya waamuzi wa soka hapa nchini.
Ongezeko la timu za wanawake linatoa ulazima wa kuwepo kwa waamuzi wanawake wa kutosha ili kuzikabili timu hizo.
Tanzania bara kuna jumla ya waamuzi wasiopungua 800 kwa ligi zote za soka lakini wanaochezesha ligi kuu bara ni 70, wamuzi wakati wapo 30 na wasaidizi 40.
ligi ya Champion ship kuna waamuzi 96, waamuzi wa kati 32 na wasaidizi 64, darada la kwanza wapo 136, wakati 64 na wasaidizi 72.
Pia kuna waamuzi 220 ambao huchezesha ligi nyengine zilizopo chini ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) kama kombe la shirikisho la Azam (ASFC) ligi ya mabingwa wa Mkoa (RCL) U-20, U-17, Wilaya na ligi ya Wanawake.
Ukiangalia nchi kama Kenya inakadiriwa kuwa na waamuzi 10,000 kwenye ligi zote huku kwenye ligi kuuina waamuzi 94 kati yao wanawake 25.
Kwa mujibu wa Mweyekiti wa kamati ya Waamuzi Zanzibar Waziri Sheha Waziri, alisema Zanzibar hadi sasa kuna waamuzi 60 (kikanda na primiya) ambapo kati yao wanwume ni wengi kuliko wanawake.
WAAMUZI
Dalila Jaffar Mtwana, Muamuzi wa mpira wa miguu na mshika bendera, alianza nafasi hiyo mwaka 2005.
kabla ya kuwa muamuzi Dalila alikua mwana riadha mashuhuri na mwana michezo mbali mbali tangu alipokua mwanafunzi wa skuli ya msingi.
Amefanikiwa kukimbia viwanja mbali mbali vya riadha ndani na nje ya Zanzibar na kufanikiwa kumaliza mita1,500, 1,600, hadi kilomita 42 na maili 30.
Alisema wakati anacheza riadha upande wa pili alikua mchezaji wa mpira, na pia kujifundisha kusimamia mpira.
Ilipofika 2005 aliingia rasmi katika nafasi ya muamuzi hivyo alianza kusoma na ilipofika 2008 akapata nafasi ya kushiriki (coopertest) vipimo vya kimataifa ambayo ilifanyika Arusha.
"Hili zoezi ni gumu kupita kiasi lakini nilipiga moyo konde kuhakikisha nafasi hiyo naipata" alisema.
Ilipofika mwaka 2015 alipata beji ya FIFA ya kuwa refarii katika mstari wa kwanza ambao kredit yake ni kubwa ukilinganisha na mstari wa pili.
"Kwa muda mrefu nilokaa toka mwaka 2008 hadi nilipopata beji ya FIFA ni takriban miaka 8 lakini sikuvunjika moyo na niliweza" alisema.
Alisema wakati huo kulikua na ugumu kiasi fulani kwani Tanzania hakukuwa na timu za wanawake walihudumia timu za wanaume pekee hadi pale walipotoka nje ya nchi.
"Hadi tulipotoka nje ya nchi ndio tulikutana na timu za wanawake wakati huo Tanzania hatukuwa na ligi za wanawake" alisema.
Jambo kubwa wanawake hawatakiwi kuwa na tamaa ya kifedha wala kimwili kwani kutashusha heshima yao na kuondoa thamni zao.
Alisema jambo jengine wanalopaswa kuliepuka waamuzi ni kujiepusha na rushwa.
Mpaka kufikia nafasi ya uamuzi changamoto nyingi alipitia ikwemo kupigwa, kutukanwa na kufukuzwa lakini hakukata tamaa.
"Kila aina ya vituko nilifanyiwa, nilipigwa, na kufukuzwa hadi kwenye viwanja, nilichafuliwa lakini sikuwahi kuitupa bendera" alisema.
Idadi ya waamuzi wanawake hairidhishi kwani wengi wameshindwa kuitumikia nafasi hiyo kwa kiasi kikubwa inahitaji moyo wa kujitoa.
Kujitolea kwake kumempa jina kutokana na madhila na shida alizopata wakati huo alipokua akichezesha mechi nne kwa siku katika viwanja tofauti na malipo yake yalikua ni shilingi 1,500 kwa mechi.
"Mechi nne kwa siku kama huna uvumilivu utaweza?kila mechi ina dakika 90, na wachezaji wote walikua wanaume"alisema.
Miaka ya sasa waamuzi hawakumbani na changamoto kama za wakati wetu, kwani hawapigwi wamewekewa ulinzi viwanjani tofauti na sisi.
Aidha alisema kwa upande wa malipo yapo vizuri, kuna madaktari ambao wanaangalia endapo utaumia.
Alisema changaomo nyengine ni waamuzi wanawake hawaoneshi utayari, wamekumbwa na tamaa, na wengine kuvaa mavazi ya nusu uchu, jambo ambalo linawaleta taswira mbaya kwa jamii.
"Fani hii wanaume wengi kuliko wanawake wanawake wasijirahisishe, na kushawishika kwani baadhi ya viongozi wanatumia nafasi zao kuwahadaa wanawake" alisema.
Miongoni mwa mafanikio yake ni kutembelea nchi mbalimbali ikiwemo Ufaransa, Kinshasa na nchi mbali mbali.
kupata nafsi ya tatu katika mashindano ya riyadha kutoka Kiwengwa hadi viwanja vya Amani na kufanikiwa kupata dola 300 mwaka 2001.
Alisema ili kupata idadi kubwa ya waamuzi wanawake lazima kuwa na msimamo ili kufikia malengo yao na sio kudanganyika kwani baadhi yao wanaanza vizuri lakini wanaishia kubeba ujauzito na kukaa nyumbani.
Sambamba na hayo alishauri serikali na wadau mbali mbali wa michezo kuwabakisha wanawake waliofanikiwa ili kuwa mfano wa kuigwa na wale wanawake wengi wajitokeze kushika nafasi hiyo.
Nae, Simai Mwinyi Kocha wa Timu ya Wizara ya Maji Nishati na Madini, alisema Zanzibar katika suala la makocha imeendelea kidogo kwani kuna vyuo vinavyotoa elimu hiyo.
Alisema ipo haja ya kusimamiwa suala hilo kwani wanaume wanaitumia fursa hiyo tofauti na wanawake.
Changamoto moja wapo ya kuwa na waamuzi wanawake ni kidogo ni kutokana na timu za kike kuwa kidogo, pamoja na timu za kiume kushindwa kufikiria kuwaita wanawake kusimamia timu zao.
"Kwangu mimi nahisi wanawake wakiamua uwezo wanao, hivyo watumie fursa kwani Zanzibar hatuna tabia ya kubaguana" alisema.
Aliwasahauri waamuzi wanawake kujitokeze kuonekana utendaji wao ili wapate nafasi kutokana na utendaji wao.
KAMATI YA WAAMUZI
Kwa mujibu wa Mweyekiti wa kamati ya Waamuzi Zanzibar Waziri Sheha Waziri, alisema Zanzibar hadi sasa kuna waamuzi 60 (kikanda na primiya) ambapo kati yao wanwume walikua wengi kuliko wanawake.
Alisema Zanziabr ina uhaba wa waamuzi ambapo kwa mwaka jana walikua waamuzi wanawake 3 tu kwa kanda.
Aidha alisema kwa mwaka huu wanatarajia kupata waamuzi wengi kutokana na hamasa baad ya kuona wenzao kufanya vizuri.
“Kwa sasa wanawake wengi wameshawishika na sisi tna uhaba wa waamuzi ambao hawatoshelezI” alisema.
Mwenyekiti alisema kuwepo waamuzi wa kike viwanjani kunashawishi wanawake wengine kusomea nafasi hiyo na hivi sasa wapo viwanjani kufanya mazoezi kwa ajili ya nafasi hiyo.
“Matarajio yetu ikifika Agosti 18 mwaka huu tutakua na mtihani kwa ajili ya kuwachagua waamuzi na wengine watapanda madaraja” alisema.
"Kufikia silimia 50 kwa 50 ni vigumu kwani wanawake wanashindwa kudumu kwa miaka mingi kwani anahitaji kuwa na familia na akishaanza kupata kizazi sio rahisi kumudu harakati hizo" alisema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) Hussein alisema nafasi za waamuzi wanawake zanzibar bado haziridhishi kwani haijafikia hata nusu ya waamuzi wanawake.
Alisema malengo yao ni kupata waamuzi bora na sio idadi kubwa ya waamuzi ingawa changamoto ipo ya wanawake kushindwa kujitokeza kwenye eneo hilo.
Aidha alisema muitikio kwa wanawake ni mdogo kwa sababu imejengeka imani kwamba huo mchezo ni wa kiume, wengi wanaogopa kujichanganya, kupigwa na kutukanwa, na kusabababisha jamii kushindwa kulikubali suala la wanawake kushika nafasi hizo.
Alisema licha ya changamoto wanazopata waamuzi wanawake viwanjani hawapaswi kukata tamaa kwani hakuna mafanikio yanayopatikana kwa rahisi.
Mara kadhaa wapo wanawake waliotia nia ya kutaka kushika nfasi hiyo lakini wanaishia njiani na wengine kuhofia kutokana na vitisho au maneno ya wachezaji.
VYAMA VYA MICHEZO
Inaelezwa kuwa idadi ya waamuzi wanawake ni ndogo kuliko wanaume na sababu mbali mbali zinahusishwa kwenye eneo hilo.
Mwanasheria Mbarouk Othman ambae Meneja wa leseni za klabu katika Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), alisema sheria ni kitu muhimu kwenye michezo ni vyema kuwepo sheria za kuwalinda ili kuondoa hofu wanawake kuchukua nafasi hiyo.
Wanawake wanapaswa kusoma ili kupata sifa za kuwa waamuzi wanaotambulika zaidi.
Alisema wapo baadhi ya wanawake wamepambana na kufanya jitihada kadhaa kuhakikisha wamepata nafasi hiyo, vijana wa sasa wanapaswa kuiga kuwa mfano wa wanawake hao.
Nafasi hiyo huipati kwa wpesi lazima ujikubalishe kuacha baadhi ya mambo yas iyo ya lazima kama kweli unataka kuwa muamuzi wa viwango na unaesifika.
WANAHARAKATI
Haura Shamte na Khatibu Suleimn ni Waandishi wa Habari wkongwe walisema mifano mizuri inayopaswa kuigwa kwa waamuzi wa soka la wanawake ni Jonesia Fukya na Tatu Malogo ambao wamepewa nafasi ya kuchezesha mechi kubwa ya simba na yanga kule Tanzania bara.
“unakuta hata ligi kuu za wanawake hapa kwetu zinachezeshwa na wanaume kutokana na uchache wa waamuzi wanawake eneo ambalo walipaswa waamuzi wanawake kuonesha umahiri wao” alisema.
Kuna tetesi zinasema waamuzi wananyimwa nafasi ya kujifungua watoto, kuolewa, kwani itashusha viwango vya o vya uchezaji
waamuzi wanawake wamekuwa wakipewa nafsi za kuchezesha mechi za soka za wanaume na hiyo imekuwa ikifanyika hata kwenye mashindano makubwa kama ya kombe la dunia la Fifa na ligi kuu ya Engalnd, michuano yenye ushindani mkubwa, wanawake wamepewa dhamana ya kuchezesha mechi hizo.
jambo hilo linafungua njia kwa waamuzi wanawake hapa nchini kwa kuongeza nguvu kwenye kuwaandaa waamuzi wa soka la wanawake wakutoosha ili siku moja kuiwakilisha nchi katika nchi za kimataifa.
Adil Mussa alisema, mafunzo ya darasani anayopewa muamuzi mwanamke na mwanamme hayana tofauti kwa sababu wote wanenda kuchezesha mpira wenye sheria sawa, (17) ingawa kwenye utimamu wa mwili kuna utofauti.
Wasichana wanaoshoriki kuchezesha michezo ya wanaume wanapaswa kukimbia katika viwango vile vile ambavyo waamuzi wa kiume wanakimbia hivyo sio jambo rahisi kwa vitendo.
Kazi hiyo inahitaji kujituma kiakili na mwili, mwili unahitaji mazoezi ya kutosha na wengi wanashindwa kwenye vitendo (cooper test) lakini kuchezesha wanaweza.
Comments
Post a Comment