UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI MASHEHA WATAKIWA KUFANYA HAYA PEMBA
Na,AMINA AHMED MOH'D- PEMBA.
AFISA mdhamini wizara ya ujenzi mawasiliano na uchukuzi Zanzibar Ibrahim Saleh Juma amewataka viongozi wa shehia kuwashirikisha wananchi katika vijiji na maeneo yao kuweza kupata maoni ya utowaji wa majina ya mitaa iliyokosewa na ambayo bado haijatambuliwa katika mfumo rasmi wa anuani za makazi (post code) ili kuweza kutambuliwa rasmi kwa ridhaa na mapendekezo ya wakazi wa maeneo husika wna kuepusha mivutano isoyo na ulazima mara baada ya kukamilika zoezi la uhakiki wa anuani za makazi kwa awamu ya pili.
Ametoa wito huo kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza nao, kufuatia ziara maalum ya kuangalia zoezi la uhakiki wa anuani za makazi linaloendelea katika shehia na maeneo mbali mbali ya mikoa miwili ya Pemba wenye lengo la kuboresha na kutambua mfumo rasmi wa makazi ya wananchi.
IBRAHIM SALEH - JUMA,A/MDHAMINI W.U.M.U -PEMBA
Amesema wapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakiendelea kulalamika juu ya kuwekwa majina wasiyoyatambua katika vibao na nguzo za utambuzi wa mitaa na maeneo yao ambayo imewekwa kwa ridhaa za viongozi wa shehia ,na kuendelea kutambuliwa majina hayo katika mifumo hiyo bila ridhaa za wanajamii husika jambo ambalo lilitokana na kukosa kushirikishwa ipasavyo wakati wa utambuzi wa awali wa uwekwaji wa vibango hivyo.
Akizungumza katika ziara hiyo mwakilishi kutoka timu ya kitaifa ya kuratibu anuani za makazi kutoka wizara ya Habari mawasiliano na teknologia ya Habari Tanzania Habari Arnold Mkude amesema lengo la uhakiki huo ni kurekebisha baadhi ya changamoto za mfumo huo zilizotolewa na wananchi ,kutokuhakikiwa kwa baadhi ya nyumba,sambamba na kuziingiza katika mfumo nyumba,mitaa na barabara ambazo hazikuwepo wakati wa uhakiki wa mwaka 2022.
Wakizungumza juu ya zoezi hilo mratibu wa anuani za makazi mkoa wa kusini Pemba Mussa Alawi Muhamed , Zena Juma Shamte sheha wa shehia ya Mtangani, Dodo,ukutini Kinowe Pamoja na baadhi ya wananchi wamesema kuwa wananchi wanaendelea kutoa mashirikiano katika kufanikisha mpango huo licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamo tofauti,ikiwemo wananchi kutokuelewa umuhimu wa zoezi hilo linaloendelea jambo ambalo hulazimika kutumia muda mwingi kuelimisha kabla ya kufanya uhakiki huo.
MUSSA ALAWI MUHAMED , MRATIBU P.CODE KUSINI PEMBA .
Ziara hiyo ya timu ya kitaifa ya kuratibu anuani za makazi kutoka wizara ya Habari mawasiliano na teknologia ya Habari Tanzania, pamoja na vongozi kutoka wizara zinazohusika na mpango huo Zanzibar zilikagua zoezi hilo katika shehia mitaa barabara maeneo mbali mbali ikiwemo ukutini mtangani, dodo,kinowe, katika mikoa miwili ya Pemba.
Mwisho,
Comments
Post a Comment