NAZAF KUNYAKUA UBINGWA MWINYI CUP
Na,Amina Ahmed - Pemba.
HATIMAE Timu ya Nazaf kutoka wadi ya Wambaa imeibuka mshindi katika tamati ya mashindano ya Mwinyi Cup iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Chambani ,ushindi ambao ulitafutwa kwa ushindani mkali wa timu 32 kutoka wadi tofauti ndani ya jimbo hilo kwa zaidi ya mwezi mmoja tangia kuanza kwa mtanange huo.
Mchuano huo wa aina yake ambao ulipigwa katika viwanja vya Mpira Mapape Chambani jioni ambapo timu hiyo ya Nazaf iliibuka ushindi wa Goli 3 kwa moja dhidi ya mpinzani na mwenyeji wake timu ya Black Mamba kutoka wadiya Dodo ambayo hadi dakika 90 za mchezo zinakamilika iliambulia goli 1 .
Timu hiyo ambayo imejinyakulia zawadi ya shilingi laki sita na 50 kutoka kwa mbunge huyo sambamba na jezi ambapo mshindi wa pili katika fainali hiyo Black mamba kukabidhiwa shilingi laki 3 na nusu na jezi huku mshindi wa tatu akipokea shilingi laki 2 na mshindi wa 4 shilingi laki 1 Taslim.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa wana michezo wa timu 32 walioshiriki mashindano hayo mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja amemshukuru mbunge wa jimbo hilo kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yamewakusanya vijana kwa pamoja katika kuendeleza michezo ambayo ni mionhoni mwa sera zinazoendelezwa kukuzwa na serikali zote mbili.
a
"Viongozi wetu wakuu wa nchi Daktari Samia Suluhu Hassan Sambamba na Dk Mwinyi wamekuwa wakituhamasisha siku hadi kufanya michezo,kitendo hichi kilichofanywa na mbunge wetu huyu wa jimbo la chambani kinaonesha kuunga mkono juhudi za viogozi wetu wakuu katika michezo kwa kuanzisha mashindano haya".
Aidha katika kuunga mkono juhudi za viongozi wakuu wa serikali ya Tanzania na Zanzibar Mjaja amesema kuwa uongozi wa wilaya hiyo ya Mkoani umedhamiria kuweka mashindano ya wilaya ambayo yatazikutanisha timu za majimbo wilayani humo kuonesha uwezo wao na kusaidia kupatikana timu moja itakayoiwakilisha wilaya katika mchezo huo maeneo mbali mbali yaTanzania.
Hata hivyo amewataka wanachambani kuendelea kuunga mkono na kuthamini juhudi zinazofanywa na viongozi wa jimbo hilo kwa kuwapa mashirikiano .
Nae Mwanzilishi wa Mashindano hayo ambae ni Mbunge wa jimbo la Chambani Muhamed Abrahman Mwinyi amesema kuwa lengo la kuanzisha michuano hiyo ndani ya jimbo hilo ni kukuza kuendeleza na na kuimarisha vipaji ili kuzifikia fursa za ajira afya na maendeleo zinazotokana na michezo .Aidha amewataka wanamichezo ndani ya jimbo hilo kujiweka tayari kwajili ya mashindano mengine ambayo yataanzishwa mwanzoni mwa mwezi wa 9 na mwezi wa 2 ambayo yataandaliwa na mbunge huyo mwakilishi pamoja na madiwani ambayo yatakuwa na zawadi bora zaidi .
Akizungumzia ushindi wa mchezo na mashindano hayo mfungaji bora katika mchezo wa fainali hiyo ya Mwinyi cup Abdalla Awesi Abdalla "Venamass " alisema kuwa hamasa ya kuibua vipaji vya mchezo wa mpira kwa vijana ndani ya jimbo hilo iliyofanywa na mbunge huyo inahitaji kuendelezwa ili viweze kufika mbali zaidi kwa kuanzishwa ligi na mashindano mbali mbali ndani ya jimbo hilo wilaya na mikoa .
Michuano hiyo ya Mwinyi cup ambayo hadi kukamilika kwake imegharimu jumla ya shilingi 10,636,000 ambapo kupitia mashindano hayo huduma za matibabu kwa wananchi waliojitokeza ikiwemo,kuchunguza afya zao kwa magonjwa yasiyowmbukiza ikiwemo,pressure,kisukari,kupata ushauri nasaha, kupima virusi vya ukimwi ,sambamba na kuchangia damu salama ziliweza kutolewa bila malipo .
Katika michuano hiyo viongozi mbali mbali wa chama na serikali walihuhudhuria kushuhudia burudani hiyo ya aina yake.
Mwisho
Comments
Post a Comment