MASHEHA MICHEWENI WAASWA HAYA NI BAADA YA KUKABIDHIWA VIFAA VYA KUTUMIA KWAJILI YA UTAMBUZI WA WANANCHI KUPITIA MFUMO RASMI WA ANUANI ZA MAKAZI KWA NJIA YA KIDIGITALI.

NA, AMINA AHMED -PEMBA.

UONGOZI WA wilaya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba umesema utaendelea kushirikiana na wananchi pamoja na kutoa elimu zaidi katika maeneo  ya miji na vijiji ndani ya shehia   zote  wilayani humo ili  waweze kuongeza uelewa  juu ya kutumia   mfumo rasmi wa   anuani za makazi kwa njia za  kidigitali na waweze kuitumia katika shughuli  zao za kila siku
               MGENI KHATIB YAHYA,  DC - WILAYA                                                 MICHEWENI
  


Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Micheweni  Mgeni Khatib Yahya alipokuwa akizungumza mara baada ya kumaliza   kukagua vifaa kazi  , vilivyokabdihiwa  na serikali  kwa viongozi  wa shehia  mbili zilizoanza majaribio  ( Pilot area )  ya mfumo huo  wa  kurahisisha shughuli za utambuzi wa anuani za makazi kwa njia ya kidigitali ghafla iliyoandaliwa na wizara ya ujenzi mawasilino na uchukuzi Pemba.

Amesema mafunzo yaliyotolewa na  waratibu wa shehia hizo juu ya  matumizi ya mfumo huo ambao unafaida nyingi katika kurahisisha upatikanaji wa huduma za maendeleo itakuwa chachu ya kukuza uelewa kwa wananchi wa shehia za wilaya hiyo   kwa kutumia mfumo huo kama ulivyokusudiwana serikali.

"Tutahakikisha elimu inawafikia wananchi na wanaitumia katikashugjuli zao zote ambazo zinahitaji utambuzi kila siku shehia zote 25 zilizopo katimawilaya hii tutakuwa 
tukipita kutowa elimu hii i kuongeza uelewa wa matumizi haya ya mfumo"

Hata hivyo Mgeni amewataka  masheha hao kutoutumia vibaya mfumo huo  na kuwanyima wananchi haki zao mbali mbali sambamba na kuwaasa kuutumia vyema vifaa hivyo  katika kuwasaidia  kuondoa mivutano  inayowakabili na  kuwatambua vyema wananchi wao waliowazunguka   kwa mujibu wa shehia zao.

"Sisi wilaya hatutokuwa tayari kuona  vifaa hivi havitumiki kwa malengo yaliokusudiwa  niwaatake masheha kuwa makini na matumizi ya hii mifumo  ili mizozo na mivutano isyo ya ulazima kwa wananchi isiweze kujitokeza kila sheha anatakiwa ajuwe wananchi wake kwa umakini mkubwa".

Aidha mkuu wa wilaya  huyo ameushukuru uongozi wa wizara ya ujenzi mawasiliano na uchukuzi Pemba kwa kuendelea  kujitolea kusimamia  kufanikisha utekelezaji wa zoezi hilo la utolewaji wa huduma za utambuzi kwa mifumo ya kidigitali   lilotokana na  dhamira njema za  viongozi wa serikali zote mbili  Tanzania za kuwarahisishia mifumo  ya upatikanaji wa huduma kwa njia  urahisi wananchi wake.

"Tuvitumie vifaa hivi kuweza kuielimisha jamii ,lakini pia kuweza kuwatambua waliotuzunguka katika shehia zetu,vifaa hivi komputer na printer pia zitumike kwa malengo yalikusudiwa"Alisema .
Akizungumza afisa mdhamini wizara ya ujenzi mawasiliano na uchukuzi Pemba  Ibrahim Saleh Juma amewataka  wasimamizi wa mfumo huo  katika shehia kuendelea kuwahakiki na kuwatambua  wahamiaji, wageni, wanaojenga   katika maeneo yao na kuwaingiza katika mfumo huo 
           IBRAHIM SALEH JUMA, A/  MDHAMINI                    WIZARA UJENZI MAWASILIANO PEMBA

Aliongeza kuwa  wizara ya habari mawasiliano na teknlogia ya habari Tanzania kwa kushirikiana na wizara ya ujenzi mawasiliano na uchukuzi Zanzibar itarudi katika shehia zilizobaki kuendeleza zoezi hilo la kuwakabidhi vifaa kama hivyo ili kuogeza maboresho zaidi katika suala hilo la anuani za makazi

"Wapo waliodhani kuwa suala hili la anuani za makazi lilitumika katika kipindi kilecha sensa tu  ,lakini wapo ambao wameshaanza kujiuliza  mbona mawasiliano wanapita tena katika suala la anuani lakini niwatoe hofu hili ni sualatu la kutqka mfumo kuwatambua kuzitambua shehia zina watu wangapinyumba ngapibarabara ngapina menginyo  kwa nia ile ile ya viongozi wetu Dk  Samia na Dk Mwinyi kupanga  na kuboresha zaidi maendeleo ".

Nao waratibu wa shehia  waliopatiwa mafunzo na vifaa hivyo wamesema kuwa wataendelea kushirikiana na viongozi hao katika kutimiza malengo yaliyokusudiwa na serikali juu ya matumizi ya mfumo huo  kwa wananchi.

Vifaa hivyo ambavyo ni Komputer,Printer   pamoja na Vish kwambi  vimetolewa kwa hatua za awali katika shehia ya Konde ,sambamba na Kinowe ambapo shehia hizo mbili  za majaribio kwa upande wa kisiwani Pemba zimeanza kutumia mfumo huo.

Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.