ZSTC YAWAONYA WAUZAJI NA WANUNUAJI KARAFUU KINYUME NA UTARATIBU ULIOWEKWA .
Na,Amina Ahmed Moh'd Pemba.
SHIRIKA la biashara la taifa Zanzibar ZSTC limewataka wakulima wa zao la karafuu kisiwani Pemba kuacha mara moja suala la uuzwaji wa karafuu kinyume na utaratubu uliowekwa na shirika hilo ili kuepusha hasara na kudhulimiwa na matapeli wanaoingia mitaani kwa njia tofauti kununua zao hilo.
Kauli hiyo kwenda kwa wakulima wa zao hilo kisiwani humo imetolewa na Sudi Said Ali mkurugenzi mwendeshaji shirika la biashara la taifa Zanzibar ZSTC usiku wa kuamkia leo alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali huko Makonyo Wawi kufuatia doria maalum ya ukaguzi na kuwatembelea wakulima wa zao la karafuu kwajili ya maandalizi ya uuzaji wa zao hilo kwa msimu maeneo mbali mbali ambayo imebaini changamoto ikiwemo kuuza zao hilo kinyume na utaratibu uliowekwa .
Amesema ununuwaji wa karafuu umewekewa utaratibu sambamba na maeneo maalum hivyo mkulima kuuza zao hilo kwa watu wasio rasmi ni kinyume na sheria huku ikiwasababishia atahari zaidi wakulima hao kutokanana kudhulimwa kwa mbinu mbali mbali na wanunuaji hao wasio rasmi.
Sudi amezitaja mbinu hizo zinazo wasababishia hasara wakulima walizozibani kufuatia doria hiyo ni pamoja na wanunuaji hao kutumia pishi kubwa zisizosahihi, mizani isiyostahili pamoja na mapolo huku wakinunua kwa baei ya chini kwa njia ya udanganyifu ukilinganisha na bei ya shirika iliyowekwa.
"Tumefanya ziara na doria hii katika maeneo mbali mbali ya kambi za karafuu lakini kwa bahati mbaya kuna wimbi kubwa la ununuzi wa karafuu ambao wa wanapita katika kambi hizo wakiwadhulumu wakulima kwa njia ya udanganyifu kwa kununua karafuu kwa pishi na tumekuta pishi tofauti tofauti wanazitumia kuwadhulumu wakulima".
"Wanunuaji hawa ambao sio rasmi wanatumia udanganyifi kuwadhulumu wakulima kwanza wanatumia pishi ambazo ni kubwa huku wakiwadanganya wakulima kuwa pishi hii ni sawa na pishi rasmi inayotumiwa, na wanunuaji ndio wanaopata faida mara mbili kwa mtindo huu huku wakulima wakidhulumiwa".
Aidha kufuatia doria hiyo shirika hilo limefanikiwa kukamata vifaa vya udanganyifu kama vile pishi,shazia mizani pamoja na karafuu kutoka kwa wanunuaji ambao walilazimika kukumbia baada ya kuwaona watendaji wa shirika hilo na kuwacha vifaa vyao huko Mtambile .
Hata hivyo mkurugenzi huyo amewataka wakulima kuhifadhi vyema karafuu zao ili kusubiri tamko rasmi juu ya ununuzi wa zao hilo kwa msimu huu itangazwe.
Ambapo kupitia mkutano huo mkurugenzi huyo akawatahadharisha wanunuaji wa zao hilo bila utaratibu uliowekwa kisheria kutokakwa wakulima kuwacha mara moja suala hilo ambapo amesema shirika halitomvumilia yeyote atakaebainika kuenda kinyume na utaratibu katika ununuaji wa karafuu.
Vifaa vilivyo kamatwa katika doria hiyo ni pamoja na pishi zenyw ujazo tofauti,shazia,mizani pamoja na karafuu kavu.
Mwisho.
Comments
Post a Comment