WANAWAKE WAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUSOMA MAFUNDISHO YA DINI .
JUMUIYA ya maendeleo ya wanawake wa kislamu Mkoa wa Kaskazini Pemba ,imetoa pongezi zake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Hussen Mwinyi kwa kuifanya siku yaa mwaka mpya wa kislamu kuwa siku rasmi ya mapumziko nchini zanzibar.
Kauli hio imetolewaa katika kongamano la maadhimisho ya mwaka mpya wa kislamu 1446 hijiria huko ukumbi wa baraza la wawakilishi wilaya ya wete Mkoa wa kaskazini Pemba.
Jumuia hio imesema imefarajika sana kuona nguvu ya dini ya kislaamu inazidi kukuwa na kukubalika ,hivyo wameomba uwamuzi huo wa rais uwe mfano wa kuigwana viongozi wengine watakaofuatia.
Akifunga kongamano hilo katibu wa baraza la wawakilishi Raya Issa amewasihi wanawake kutafuta elimu ya dini na kidunia ili kuwasaidia kujitatulia changamoto mbalimbali katika jamii.
Katibu huyo amewasihi wanajumuia hio kusimamia vyema malezi kwa watoto wao na kupiga vita matendo ya udhalilishaji yanayoongezeka siku hadi siku.
Akisoma risala ya jumuia hio ukhti Asha Ali Sleman amesema moja ya malengo makubwa ya jumuia ni kuhakikisha wanawake wote inawafikia elimu sahihi ya dini ya kislamu huku wakifahmisha malezi bora yenye kufuata misingi na maadili ya dini ya kiisalmu .
Jumla ya mada tatu zimewasilishwa katika kongamano hilo ,huku likibeba ujumbe usemao hadhi ya mwanamke nikupata elimu ,ewe mwanmke hudhuria madrasa .
Mwisho
Comments
Post a Comment