WANANCHI KISIWA CHA KOJANI WALILIA KUKOSA MADAKTARI KITUO CHAO CHA AFYA

Na - AMINA AHMED, PEMBA.
AKINA MAMA KATIKA KISIWA CHA Kojani mkoa wa Kaskazini Pemba wameiomba serikali ya mkoa kuwasaidia kulipatia ufumbuzi suala la  uhaba wa madakatari pamoja na wauguzi katika kituo chao cha Afya ili kuweza kuondokana na usumbufu wanaokutana nao  hususan ni mama  wajawazito.

Wametoa ombi hilo walipokuwa wakizungumza  mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa  huo uliofika kisiwani humo kusikiliza changamoto zinazowakabili  wananchi  ndani ya kisiwa hicho mapema leo.

Wamesema  kituo cha afya ndani ya kisiwa hicho kina daktari mmoja ambae  wakati mwengine  kushindwa kutoa huduma kwa baadhi ya kesi za matibabu zinazofika kituoni humo huku akilazimika kutoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 80 kwa siku .

Aidha wameomba kupatiwa ufumbuzi wa changamoto  ya kukosa  maji  safi katika baadhi ya maeneo iliyokosekana kutokana na  kuharibika kwa muda mrefu tangi lilikokuwa likisambazia maji katika maeneo mbali mbali ya vijiji hivyo  .

Katika hatua nyengine wananchi hao wameiomba serikali ya mkoa kuwasaidia kudhibiti mmonyoko wa maadili  kwa kuridhia sheria zitakazowekwa na kamati ya maadili kisiwani humo  .
  RC - KASKAZINI  ,SALAMA MBAROUK KHATIB.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kaskazini Pemba ambae pia ni mkuu wa mkoa huo  Salama Mbarouk   Khatib  amesema kuwa ataendelea kulifanyia kazi suala hilo kwa kulifikisha kwa uongozi wa wizara ya afya ili kuona linapatiwa ufumbuzi wa haraka na uongozi wa wizara ya afya  kwa maslahi ya wananchi.

Aidha amewataka akina mama wa kisiwa hicho  kujifungulia hospitali sambamba na kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito  ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza endapo watajifungulia majumbani  mwao.

Akijibu kuhusu changamoto ya upatikanaji wa huduma  ya maji safi na salama mkuu huyo aliwahakikishia wananchi hao kuwa suala  hilo litapatiwa ufumbuzi  siku ya jumamosi ni baada ya kuzungumza hadharani kwa njia ya simu  uongozi wa mamlaka ya maji Zanzibar zawa na kutoa ahadi hiyo.

  Aidha akizungumzia suala la maadili mwenyekiti huyo amewataka wazazi kusimamia na kufuatilia mienendo ya vijana na watoto ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo viouvu.

 Katika hatua nyengine  Rc Salama ameagiza kukatwa nywele  kwa vijana wakiume  wanaofuga na kusokota  rasta, kuvaa nguo za kubana na kuzishusha suruali zao sambamba na kuwataka kuacha mara moja tabia hizo ambapo amesema pia uongozi wa mkoa utawashughulikia ipasavyo  
 ili kurudisha nidhamu ya maadili.


 Hata hivyo akina mama hao wamemshukuru Rais wa Zanzibar  Dk Hussein Ali Mwiny kwa kuendelea kuleta mageuzi makubwa ya kkimaendeleo ndani ya mkoa hu ikimo kisiwa cha kojani.
Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.