TEEMO YALETA FARAJA KWA WANAFUNZI SKULI ZA MSINGI PEMBA YAAHIDI KUIENDELEZA TANZANIA NZIMA .
NA,AMINA AHMED MOH'D, PEMBA.
SHIRIKA lisilo la kiserikali Tanzania Environment and Empowerment
( TEEMO ) leo limezindua rasmi kampeni maalum ya ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wa skuli za Msingi nchini ijulikanayo kwa jina la "School bag for Batter Tomorrow" kwa kugawa vifaa ikiwemo, mikoba,mabuku Penseli pamoja na raba .
Akizungumza na wanafunzi wa Sizini msingi katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyodhaminiwa na Shirika la CEAMSA kutoka Spain pamoja na CWEEDMWANI Tanzania
Mkurugenzi wa Teemo Winfrida Jackson Shonde amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwasaidia wanafunzi wote wa Tanzania kupata vifaa Muhimu na kuongeza ijasiri wa kufanya vyema katika masomo yao pamoja na kuongeza uelewa kutunza mazingira .
Amesema mikoba hiyo itasaidia kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo kwa asilimia nyingi hutimiwa na wanafunzi kubebea vifaa vya skuli na kuharibu mazingira hivyo TEEMO kupitia kampeni hiyo itaendelea kushirikiana na serikali zote mbili katika kutimiza malengo yaliyowekewa juu ya mazingira bora na wezeshi kwa wanafunzi .
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya CWEED Mwani Kanda ya Pemba GERRY SCANDER amesema zoezi la ugawaji wa mikoba na vifaa hivyo linalofanywa na TEEMO kwa skuli za Pemba litasaidia wanafunzi kupata mabegi bali litaongeza motisha na kufanya vyema wanapokua skuli.
Wakizungumza baadhi ya wanafunzi waliopatiwa vifaa hivyo wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia msaada huo ambapo wamesema awali walikuwa wakitumia mifuko kutilia vifaa vya skuli huku mwalimu mkuu wa skuli hiyo Sleiman Abdalla Khamis ameipongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kuzisadia jamii katika harakati mbali mbali za maendeleo .
TEEMO kwa Kushirikiana na CWEEDMWANI pamoja na CEAMSA imetekeleza kampeni mbali mbali ikiwa ni pamoja na kampeni ya WEZESHA WASICHANA ,MKULIMA WA MWANI BALOZI WA MAZINGIRA na nyengine mbali mbali ambapo Kampeni hii ya School bag for better tomorrow iliyozinduliwa leo inaendelea katika skuli mbali mbali kisiwani humo .
Mwisho.
Comments
Post a Comment