SERIKALI YA MKOA KUTOA UAMUZI WA MWISHO ENEO LA UJENZI WA SOKO KISIWA CHA KOJANI .

Na ,AMINA AHMED MOH'D

MKUU WA mkoa wa kaskazini Pemba Salama  Mbarouk Khatib amesema kuwa uamuzi wa mwisho utatolewa na  serikali ya mkoa  juu ya eneo  litakalojengwa soko  la  wafanya biashara ndani ya wilaya ndogo ya Kojani .


Ameyasema hayo leo mara baada ya kumaliza kupokea maoni ya wananchi  ndani ya kisiwa hicho ambayo yalishindwa kutoa maamuzi  kufuatia  mvutano baina ya wananchi  wenyewe kwa wenyewe kutaka kujengwa soko maeneo manne tofauti ndani ya kisiwa hicho katika mkutano maalum uliofanyika  katika uwanja wa Kojani mji mpya.

Amesema  baada ya kupata maoni hayo ya wananchi serikali itatoa uamuzi  utakaoendana na vipimo vya kitaalamu  juu ya eneo litakalofaa kujengwa soko hilo litakalowasaidia wananchi kuuza biashara zao maeneo yalio rasmi .

Aidha  mkuu huyo amewataka wananchi wa kisiwa hicho kuacha mivutano isiyo na  tija  yanapokuja masuala ya maendeleo   kwa maslahi mapana ya wananchi wa kisiwa hicho.

Awali akizungumza kwa niaba ya mkuu wa  wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahya ambae ni mkuu wa wilaya ya Micheweni amewataka Wananchi hao kuunga mkono juhudi za rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi  katika kuleta maendeleo  kwa wananchi wake maeneo mbali mbali.

Awali wakizungumza Baadhi ya wananchi wameiomba serikali  kuzingatia maslahi mapana  ya wananchi watakapochagua eneo la ujenzi huo .

Mkutano huo uliowajumuisha   wananchi wa shehia za kojani ,kamati za ulinzi na uslama  mkoa wa kaskazini,watendaji wa baraza la mji Wete , pamoja na viongozi wa  jimbo hilo la kojani.

  
 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.