MWAMUZI WA KIKE PEMBA ALILIA KUKOSA FURSA KATIKA MICHEZO PAMOJA KUBAGULIWA .
Na AMINA AHMED MOH'D PEMBA.
"SISI waamuzi Pemba tunabaguliwa,hatushirikishwi, hatupewi fursa licha ya kuwa zipo ,tunakosa kujifunza, hatulipwi, vitendea kazi hatuna ,serikali kama imetuwacha nyuma haituangalii,,tunatukanwa, vifaa vya mazoezi hatuna, mtu ile flana anavaa mpka dakika za mchezo zinakwisha habadilishi,Ligi zile za serikali silipwi Kuna siku nauli nakosa kuja mazoezi nadandia tu lifti".
"Nikifika uwanjani nafanya majukumu ambayo sio yangu sionekani kama mwamuzi naonekana mtu wa kawaida tu,mara niokote mipira mara niwapelekee watu maji ilimradi sionekani wa hadhi kama waamuzi wengine hususan ni huku kwetu Pemba,ingawa sivunjiki moyo ilani vitu ambavyo natamani vipatiwe ufumbuzi ".
Yote hayo ni maneno kutoka kwa Safia Khamis Ali mwamuzi wa kati ( centa refa ree ) katika mchezo wa mpira wa miguu kisiwani Pemba ambae licha ya changamoto hizo na nyengine mbali mbali hajawahi kuchoshwa na kazi yake hiyo akiamini siku moja Changamoto hizo zitabaki kuwa hadithi .
Safia, mkaazi wa Kianga Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba ambae kwa mapenzi yake aliamua kuipigania nafasi hii katika michezo, ambapo kwa sasa ana zaidi ya miaka 2, ni baada ya kujiona anauthubutu ,ujasiri na utayari wa kuitendea kazi hiyo huku michezo ikiwa kwenye damu akiianza akiwa skuli.
Alianza kujifunza uamauzi kwa kuangalia wengine katika uwanja Gombani, kwenye runinga kupitia ligi mbali mbali zinaoneshwa na baadae kupata mafunzo ya vitendo katika uwanja wa Polisi Madungu huku mwalimu wake Akiwa Muhamed Amour Mwalim ( MD ) .
Safari ya kujifunza uamuzi haikuishia hapo Safia pia alilazimika kusafiri kutoka Pemba kwenda Unguja na huko pia alipata mafunzo kupitia baadhi ya waamuzi wa michezo wa kisiwa hicho akiwemo Ali Kibo, pamoja na mwalimu Issa.
Baada ya kurejea tena kisiwani Pemba kazi ya kujifunza iliendelea ambapo mwalimu wa awali pamoja na mwalimu mwengine waliendelea kumjenga Safia kwa kumfundisha Safia aliekuwa na dhamira ya kuwa muamuzi .
Mafunzo ya vitendo na mazoezi kwa muda mrefu kutoka kwa walimu wenye uzoefu waliomfunidisha Safia yaliweza kuzaa matunda ni baada ya mama huyo kufanya mtihani ambao ili kutambulika rasmi kama mwamuzi ni suala la lazima kuufanya.
Mtihani huo wa Coper test haukumuwia ugumu Safia na alifanya vizuri na yeye kuwa mwanamke peke yake kisiwani Pemba aliyeweza kupata nafasi hiyo ya kuwa mwamuzi wa kati kati wote waliofanya mtihani ambao wote walikuwa ni wa kiume.
Harakati za kuchezesha mechi ndogo ndogo za cen central zilianza ambapo hatoweza kuisahau mechi zake 4 za kwanza kuziamua akiwa mwamuzi wa kati katika viwanja vya Tibirinzi,Fufuni ,Kangani, huku mechi kubwa ligi daraja la kwanza na daraja la pili akiamua katika kisiwa cha Unguja Uwanja wa Mau A na B nilipata pongezi nyingi licha ya kuwa ni mara ya kwanza.
Safia ambae umri wake ni miaka 34 mama mwenye mtoto mmoja,mlezi wa baba mama na familia yake kupitia harakati hizo za michezo na nyengine anazozifanya anahudumia vyema familia yake katika harakati za kila siku .
Jamii inayomzunguka Safia imempokea kwa mitazamo tofauti ikiwa wapo ambao wanaamini uamuzi na michezo kwa mwanamke ni jambo ambalo sio sahihi huku wengine wakilichukulia suala hilo ni kuwa la kawaida huku yeye mwenyewe akiamini kuwa maamuzi yake ya maisha juu ya kile anachokipenda yana muhusu mwenyewe sio mtu mwengine .
Zulfa Shaame Ali anasema kuwa mara nyingi anamuona Safia akijishughulisha na harakati za michezo ambapokwa upande wake anachukulia suala hilo analolifanya mwamuzi huyo kuwa ni kujitoa ufahamu ili kutimiza mahitajio yake.
" Naamini anajichetua na kujifaya chakaramau tu ili kujipatia kipato cha kuendesha familiayake lakini sio kazi mbaya kama anapata kipato ,na muhimu anajistiri bhasi lakini mimi kama mimi sitaki hata siku moja kusema nikaachanganyike na kundi la wanaume eti nachezesha mpira watu wote wananiangalia mimi".
Kwa upande wa familia yake ambayo ni mama,kaka pamoja na baba mzazi wa Safia wanamuunga mkono kwa vile mama huyo anakidhi mahitaji yake ya mtoto na familia yake ingawa awali baba yake mzazi hakuonesha kupendezewa na suala hili kwa kilealichokihofia kuwa anaweza kubadilika tabia.
"Awali baba yangu alikuwa hataki nijichanganye na masuala ya michezo nikiwa skuli mama yangu ndio alikuwa ananiibia kuniagia naenda kushiriki ,lakini kadri siku zilivyozidi ilw hamasa ya kupenda michezo kwangu haijawahi kupungua nilikuwa naenda Gombani kuangalia mpira kila jioni na ndipo aliponiunga mkono nashukuru hajawahi tena kuacha kunisapoti kwa lolote lile".
Mimi ni mama ambae najichumia mwenyewe na nina mtoto mgonjwa wazazi wangu pia wananitegemea kwa vile na wao ni watu wazima natofautisha muda wa michezo na majukumi yangu ya nyumbani,ikiwemo kumpeleka mwanangu skuli, kupika na kufanya shughuli nyengine za nyumbani na wala hakuna amabacho kinaharibika na michezo kwangu mara nyingi ni jioni.
Mpambanaji huyu ambae licha ya kuwa ni mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu ,lakini pia nje ya michezo anajishughulisha na kazi mbali mbali ikiwemo kushona ,pamoja na kufanya biashara ndogo ndogo .
Muhamed Amour Mwalim (MD) ni mwamuzi wa mpira wa miguu kanda ya Zanzibar ambae pia ni mkufunzi wa uamuazi kwa wanafunzi mbali mbali anasema kuwa alimfahamu Safia viwanjani kwa kuwa mwanamke ambae aliiona nia yake ya michezo jambo balo halikumuia ugumu kumfundisha Uamuzi wa soka alipomuomba kumsaidia suala hilo.
MOHAMED AMOUR MWALIM (MD ) MWAMUZI, MPIRA WA MIGUU KANDA YA ZANZIBAR.
" Niko na wanafunzi wengi rika tofauti na kwa sasa niko na wanafunzi sita ambao wote wako katika standad nzuri ya kuhakikisha wanafanya maamuzi sahihi ya kuzitafsiri sheria 17 za mpira wa miguu,na actual safia ni mwanafunzi wangu kweli na mara nyingi nilikutana nae humu humu viwanjani kuna siku tunakimbia nakumbuka akanifata akaniomba nimfundishe uamuzi kwa vitendo nikamfundisha na wezake ambao ni wanaume huku mwanamke akiwa yeye peke yake tangia nimeanza kuwafundisha wanafunzi na alikuwa na utayari".
Anafanya vizuri na mimi niwaambie wazazi fursa zipo wasiwanyime watoto wakike uhuru kwa sababu zisizoeleweka mpira ni ajira mpira ni fursa kama mavazi ndio tatizo hakuna sheria inayo muamuru mwanamke kuvaa nusu uchi nimaamuzi ya mtu mwenyewe"
Ni kweli bado wanawake huku kwetu wapo nyuma katika michezo na mfano ni huyu safi mimi nishafadisha wengi lakini kwa mwanamke ni yeye peke yake Na mimi sitosita kumfundisha yeyote ambae atakuwa na utayari nipo tayari mda wote nawakaribisha katika kuona tunaongeza usawa na ushiriki wa kijinsia katika michezo "
Kassim Juma Salum ni katibu wa mpira wa miguu kwa vijana ( central ) wilaya ya Chake chake anasema anamuona mbali Safia endapo changamoto anazokumbana nazo katika viwanja na kujengewa uwezo zitapatiwa ufumbuzi na wadau wa soka.
" Tunamtumia sana katika michezo yetu na kiukweli ni mwamuzi mzuri, anauwezo wa kukimbia na kuzitafsiri sheria 17 za mpira ipasavyo ni mwamuzi hana utofauti na hao wanaume katika kutekeleza jukumu lake hilo ,kuhusu changamoto ni za kawaida endapo atawezeshwa ipasavyo ataweza kufika mbali zaidi "
Safia anasema kuwa michezo haiondoi stara na heshima ya mtu ambayo mwenyewe ataamuwa kujiwekea huku akiamini kuwa mavazi pia ni maamuzi mabaya ni mtu mwenyewe binafsi mimi navaa stoking refu, tight,kilemba na suruali refu bodi suti na wala hakuna anaeona mwili wangu .
" Ukweli ni kwamba changamoto ni nyingi kwanza tunatukanwa bado hakuna elimu ya michezo timu ikifungwa mashabiki wanakutukana matusi ambayo hata wazazi wao hawawezi kukubali endapo watatukanwa bila hata kupimwa.
" Uamuzi kwetu bado hauonekani wa thamani sio kwa mwanaume wala wanawake sisi wanawake ndio tumezidi hatushirikishwi tunazisikia tu fursa za michezo wanapelekewa watu ambao hata hawastahiki mifano mingi ipo".
"Muamuzi unaweza ukachezesha mechi ambayo unajipa matumaini hii utapata walau pesa ya daladala lakini wapi mpka leo kuna mechi tumechezesha hatujalipwa tena za serikali kombe la mapinduzi, na hata yale maji hatujapewa tumedai mpaka tumesamehe "
Vifaa kama jezi hatuna pia ,sishirikishwi nadra sana kupewa fursa niamue mechi , nathubutu kujiita muamuzi kwa vile nimepata elimu na nina ule utayari lakini hata vile kupewa kujaza fomu bhasi sipewi nakata tamaa lakini najipa moyo lakini mambo magumu ndio mana najikeep bussy na mambo mengine huku tunalegeza kamba kwa sababu hakuna maslahi fursa wanakula wengine"
Vifaa kama becon,Jezi,mipira,suruali,viatu, mafunzo kushirikishwa vyoote tunakosa yaani tupo nya sana michezo haionekani kama ni ajira kwa upande wetu"
Nina ndoto za kufika mbali sana kimichezo natamani siku moja niamue mechi zenye ushindani ,kimataifa na kitaifa kwa sababu uwezo ninao wadauwa michezo serikali na wapenda maendeleo kwa wanawake msiache kuniunga mkono uwezo ninao na uthubutu pia ".
Safia anasema kuwa si tu uamuzi wa mchezo wa mpira lakini pia utayari wake upo hata kwa kufundisha wengine michezo ,na kushiriki yeye mwenyewe ni miongoni mwa vitu alivyo na uthubutu navyo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment