KOJANI WATOA 5 KWA DK MWINYI
NA, AMINA AHMED MOH'D- PEMBA.
WAKAZI wa wilaya ndogo Kojani wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba wamempongeza rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuimarisha sekta ya elimu ambapo wamesema hatua za mwisho za ujenzi wa skuli ya kisasa inayoendelea kujengwa kisiwani humo itasaidia kuleta maendeleo katika nyanja tofauti.
Wametoa shukrani hizo walipokuwawakizungumza na habari hizi kufuatia ziara maalum ya kukagua miradi ya maendeleo wilaya ya Wete iliyoandaliwa na viongozi wa baraza la vijana Zanzibar ,iliyowakutanisha viongozi wa mabaraza hayo Unguja na Pemba mapema leo .
Wamesema kuwa juhudi za kusogeza maendeleo zaidi zinazofanywa na Dk Mwinyi ndani ya kisiwa hicho ikiwemo miundo mbinu bora ya elimu itasaidia kuendeleza na kuibua vipaji na vipawa katika fani mbali mbali ambavyo vitaendeleza kisiwa hicho.
Wamesema maendeleo hayo yamekuwa faraja kubwa kwa wakaazi na wazawa wa kisiwa hicho ambapo wameona kukuwa na kubadilika kimaendeleo katika kipindi cha muda mfupi.
"Muonekano wa kisiwa cha kojani umebadilika umekuwa mzuri yaani mandahari imebadilika tumejengewa majengo haya ya skuli za kisasa ya ghorofa
"Rais wetu katufanyia kitu ambacho ni kikubwa sana ndani ya kisiwa hichi hatujawahi kufikiria kama kuna siku tutakuwa na skuli za kisasa,uwekezaji huu uliofanywa kwa moyo wa upendo kutoka kwa kiongozi huyu umetupa imani kubwa sana hatujui tueleze vipi furaha yetu kwa hili naamini watoto wetu watasoma katika mazingira mazuri bila ya usumbufu ule wa kuvuka na kurudi "
"Tutaweza kutoa vipawa mbali mbali hapa ,madaktari,waalimu, wavuvi wa kisasa ,wafanya biashara wazuri,ambao wao watakuwa msaada katika kuendeleza zaidi maendeleo ndani ya kisiwa chetu lakini pia sehemu tofauti ndani ya taifa letu"Alisema Hamida Mussa Shabani mkazi wa Kisiwa cha Kojani.
Kojani kwa ujumla tumefarijika sana sana sana kwa,hatujaona mfano bora kama wewe mwenyezimungu akulinde ampe maisha marefu ili kizazi chetu cha sasa na kitakachokuja kifaidike na jengo hili na mengine ,kiukweli umekuwa ni mfano bora kwa wakojani kutujwngea jengo la pili la ghorofa tunaiomba wizara kuziendeleza jitihada hizi kwa kutuwekea boding ili watoto wetu waweze kusoma kwa uzuri na utulivu zaidi muda wote bila kuenda sehemu nyengine"
Aliongeza Bikombo Chumu Hamad .
Kwa Upande wake Mwalimu Mkuu skuli ya Kojani Msingi B, Asaa Nshazume Sheha amesema kuwa kabla ya jengo hilo wanafunzi ndani ya kisiwa hicho walikabiliwa na changamoto ya kubwa ya idadi ya wanafunzi na uchache wa nafasi za kusomea katika madarasa .
ASAA NSHAZUME SHEHA, M/MKUU KOJANI MSINGI.
"Tunaamini siku chache zijazo changamoto kwa wanafunzi wa skuli za msingi Kojani zitaondoka ,mpka saivi tuko wanafunzi 2008 ambao tunalazimika kugawa shifti mbili kwa sasa tunaamini hili litakwenda kuondoka hivi karibuni".
Nae Kwa upande wake Hamad Ali Bwakame Sheha wa shehia ya Kojani amesema kuwa kitendo cha Dk Mwinyi kukiangalia kwa ukaribu zaidi kisiwa hicho katika kusogeza maendeleo kimeongeza imani zaidi kwa wananchi juu ya uongozi wake, ambapo amewataka wananchi ndani ya kisiwa hicho kuendelea kutunza na kuyalinda majengo hayo ili yaweze kutumika kwa muda mrefu mara yatakapoanza kutumiwa .
Ujenzi wa skuli hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya rais Dk Hussein Ali Mwinyi aliyoiahidi kwa wananchi wa kisiwa hicho cha Kojani tarehe 22/7/2022 kuwajengea skuli ya msingi ya kisasa ambayo itaondoa changamoto ya mrundikano wa wanafunzi madarasani na kuondoa utaraibu wa kuingia mikumbo miwili wanafunzi wa skuli ya msingi ambapo jengo hilo lililokamilika ujenzi wake kwa asilimia 99 lina jumla ya vyumba 32 .
Mwisho.
Comments
Post a Comment