KOJANI WATOA 5 KWA DK MWINYI




NA, AMINA AHMED MOH'D- PEMBA.


      JENGO LA KISASA SKULI YA MSINGI KOJANI
    MUONEKANO WA NJE JENGO LA SKULI MPYA KOJANI,  PICHA NA AMINA AHMED.
WAKAZI wa  wilaya ndogo Kojani wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba wamempongeza rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuimarisha sekta ya elimu  ambapo wamesema  hatua za mwisho za ujenzi wa skuli ya kisasa  inayoendelea kujengwa kisiwani humo itasaidia kuleta maendeleo katika nyanja tofauti.

Wametoa shukrani hizo walipokuwawakizungumza na habari hizi kufuatia ziara maalum ya kukagua miradi ya maendeleo wilaya ya Wete iliyoandaliwa na  viongozi wa baraza la vijana Zanzibar ,iliyowakutanisha viongozi wa mabaraza hayo Unguja na Pemba mapema leo .
  Wamesema kuwa juhudi  za kusogeza maendeleo zaidi zinazofanywa na Dk Mwinyi ndani ya kisiwa hicho ikiwemo miundo mbinu bora ya elimu itasaidia kuendeleza na kuibua  vipaji  na vipawa katika fani mbali mbali ambavyo vitaendeleza kisiwa hicho.

Wamesema maendeleo hayo yamekuwa faraja kubwa  kwa wakaazi na wazawa wa kisiwa hicho  ambapo wameona kukuwa na kubadilika kimaendeleo  katika kipindi cha muda mfupi.

"Muonekano wa kisiwa cha kojani umebadilika umekuwa  mzuri yaani mandahari  imebadilika tumejengewa majengo haya ya skuli za kisasa ya ghorofa 

"Rais wetu katufanyia kitu ambacho  ni kikubwa sana  ndani ya kisiwa hichi hatujawahi kufikiria kama kuna siku tutakuwa na skuli za kisasa,uwekezaji huu uliofanywa kwa moyo wa upendo kutoka kwa kiongozi huyu umetupa imani kubwa sana   hatujui tueleze vipi furaha yetu kwa hili naamini watoto wetu watasoma katika mazingira mazuri  bila ya usumbufu ule wa kuvuka na kurudi "

"Tutaweza kutoa vipawa mbali mbali hapa ,madaktari,waalimu, wavuvi wa kisasa ,wafanya  biashara wazuri,ambao wao watakuwa msaada katika kuendeleza zaidi maendeleo ndani ya kisiwa chetu lakini pia sehemu tofauti ndani ya taifa letu"Alisema Hamida Mussa Shabani mkazi wa Kisiwa cha  Kojani.

Kojani kwa ujumla tumefarijika sana sana sana kwa,hatujaona mfano bora  kama wewe mwenyezimungu akulinde ampe maisha marefu ili kizazi chetu cha sasa na kitakachokuja kifaidike na  jengo hili na mengine   ,kiukweli umekuwa ni mfano bora kwa wakojani kutujwngea jengo la pili la ghorofa  tunaiomba wizara kuziendeleza jitihada hizi kwa kutuwekea boding  ili watoto wetu waweze kusoma kwa uzuri na utulivu zaidi muda wote bila kuenda sehemu nyengine"
Aliongeza  Bikombo Chumu Hamad  .

Kwa  Upande wake Mwalimu Mkuu skuli ya Kojani Msingi B,  Asaa Nshazume Sheha amesema kuwa kabla ya jengo hilo  wanafunzi ndani ya kisiwa hicho walikabiliwa na changamoto ya kubwa ya idadi ya wanafunzi na uchache wa nafasi za kusomea katika madarasa .
  ASAA NSHAZUME SHEHA, M/MKUU KOJANI                                 MSINGI.
"Tunaamini siku chache zijazo changamoto kwa wanafunzi wa skuli za msingi  Kojani zitaondoka ,mpka saivi tuko wanafunzi 2008 ambao tunalazimika kugawa shifti mbili kwa sasa  tunaamini hili litakwenda kuondoka hivi karibuni".

Nae Kwa upande wake Hamad Ali Bwakame Sheha wa shehia ya Kojani  amesema kuwa   kitendo cha Dk Mwinyi kukiangalia kwa ukaribu zaidi kisiwa hicho katika kusogeza maendeleo  kimeongeza imani zaidi kwa wananchi juu ya uongozi wake, ambapo amewataka wananchi ndani ya kisiwa hicho kuendelea kutunza  na kuyalinda majengo hayo ili yaweze kutumika kwa  muda mrefu mara yatakapoanza kutumiwa .

 
Ujenzi wa skuli hiyo ni utekelezaji wa  ahadi ya rais Dk Hussein Ali Mwinyi aliyoiahidi kwa wananchi  wa kisiwa hicho  cha Kojani  tarehe 22/7/2022  kuwajengea  skuli ya  msingi ya kisasa ambayo itaondoa changamoto ya mrundikano wa wanafunzi madarasani na kuondoa utaraibu wa kuingia mikumbo miwili wanafunzi wa skuli ya msingi   ambapo jengo hilo lililokamilika ujenzi wake kwa asilimia 99  lina jumla ya vyumba 32 .

Mwisho.



  

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.