BONANZA LA AINA YAKE KUFANYIKA PEMBA SHAMRA SHAMRA KUANZA KESHO .

NA AMINA AHMED,PEMBA.
 CLUB ya mazoezi ya viungo Gombani fitness kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar pamoja na shirika la Bima Zanzibar  ZIC wameandaa bonanza  la michezo na mazoezi kisiwani Pemba litakaloanza  shamra shamra zake kuanzia kesho tarehe 20   na kufikia kilele siku ya tarehe 28 Mwezi huu kwa kufanyika matembezi ambapo  zaidi ya washiriki 500 kutoka  nje ya kisiwa cha Pemba wanatarajiwa kushiriki katika bonanza hilo.
     KHALFAN AMOUR, MRATIBU WA BONANZA .

Akizungumza Mratibu wa Bonanza hilo KHalfan Amour Muhamed  ambae pia ni katibu wa Gombani fitness amesema kuwa lengo Bonanza hilo   litakaloanza  na matembezi kutoka  Madungu  hadi uwanja wa  Gombani   kuanzia saa 12 za asubuhi ni  kusaidia kuhamasisha ushiriki wa  wanawake na wasichana  kwa  kushirikisha na kukuza usawa wa kijinsia katika  michezo ya aina mbali mbali   kwa wanawake kisiwani humo .

Amesema Club hiyo kwa kutambua juhudi zinazofanywa na wadau wa michezo kwa wanawake wameona kuna umuhimu mkubwa  wa kulitumia bonanza hilo la miaka kumi kuunga mkono na kuhamasisha kukuza usawa wa kijinsia katika michezo kwa kuwashirikisha viongozi mbali mbali wa serikali  taasisi binafsi pamoja na wananchi   kutoka maeneo tofauti.

Aidha mratibu huyo amesema kuwa  jumla ya michezo mitatu inatarajiwa kuchezwa katika   siku ya kilele cha maadhimisho hayo ambayo ni pamoja na mchezo wa mbio za magunia ,mchezo wa kuvuta kamba pamoja na mchezo wa mazoezi  ya viungo ambayo itashirikisha jinsia zote katika kuonesha vipaji vyao walivyo navyo.

Akizungumzia kuhusu shamra shamra  zitakazoanza kesho mratibu huyo amesema kuwa waandaaji wa bonanza hilo wamedhamiria kupita katika maeneo mbali mbali kutoa elimu kwa jamii, na kuhamasisha usawa wa kijinsia  katika mazoezi na  michezo,sambamba na kutoa elimu juu ya kujikinga na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi na wasichana kupitia  mbinu mbali mbali za michezo.


Kwa upande wake mratibu wa Tamwa Pemba Fat-hiya  Mussa Said amesema kuwa lengo la chama hicho  kuunga mkono juhudi  za club hiyo katika maadhimisho ya kutimiza miaka 10  ni kusaidia kuongeza uelewa kwa jamii juu ya  umuhimu wa michezo kwa maendeleo.
   FAT-HIYA  MUSSA ,MRATIBU TAMWA PEMBA.
Aidha amewataka wananchi maeneo mbali mbali kujitokeza kushiriki na kuangalia  k michezo ya vol ball,basket ball pamoja na mpira wa miguu  itakayozikutanisha timu mbali mbali za wanawake pamoja na wanafunzi  itachezwa katika viwanja tofauti  kufuatia shamra shamra za bonanza hilo .

Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa shirika la Bima Zanzibar ofisi ya Pemba Khatib Bakar alisema, lengo la Bima ni kumrejesha mtu katika hali yake hivyo, aliwashauri wanamichezo kukata bima ambazo zitawarejesha pale ambapo walikua kabla ya kupata majanga.
        KHATIB  BAKAR, ZIC PEMBA.

  Kupitia  Bonanza hilo  ambalo limebeba kauli mbiu ya  "WEKEZA KATIKA MAZOEZI NA MICHEZO KWA JINSIA ZOTE" huduma za kujiunga na bima  za majanga mbali mbali pamoja na elimu juu ya  bima zinazotolewa na   ZIC zitatolewa.


Mwisho







Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.