ANAEDAI KUDHULUMIWA HAKI YAKE NA JESHI LA POLISI AMLILIA RAIS DKT SAMIA AMSAIDIE .
NA , AMINA AHMED MOH"D - PEMBA.
MZEE Masoud Hamad Omar mkaazi wa Wete mkoa wa Kaskazini Pemba amemuomba na amemlilia rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kumsaidia kupata haki yake anayodai kunyimwa kwa uonevu na jeshi la Polisi Tanzania .
Kilio cha mzee huyo kwenda kwa mtetezi wa wanyonge daktari Samia Suluhu Hassan amekitoa leo alipokutana na waandishi wa habari kisiwani Pemba kwa lengo maalum la kutaka wamsaidie kuyafikisha malalamiko yake kwa kiongozi huyo mkuu aliyodai licha ya kusubiri kwa muda mrefu na kufuatalia haki yake aliyodhulumiwa na Jeshi hilo ameshindwa kumfikia .
Akiongea kwa masikitiko mzee huyo amesema kuwa uonevu aliofanyiwa na jeshi hilo ni kusimamishwa kazi kwa kosa la kutokwenda kazini siku mbili kutokana na kuumwa na matatizo ya wasi wasi alioyoyapata akiwa katika vitani nchini Uganda.
Mh rais kwa heshima kubwa naomba unisaidie kupata haki zangu kutoka jeshi la Polisi , Mimi nilikuwa mfanya kazi wa jeshi la polisi kuanzia mwaka 10/ 5 /1973 na nilisimamishwa kazi mwaka 1980 kwa kosa la kutokwenda kazini siku mbili bila kupewa barua na nilikaa kusubiri kurejeshwa lakini mpka mwaka 2002 sikurudishwa nikaamua kuomba barua ya kustaafu kwa hiari kwa vile hali yangu ya ugonjwa bado ilikuwa haijatengamaa lakini pia jeshi hilo lilinyamaza kimya hawakunijibu chochote nikarudia tena mwezi wa 12 pia wakanyamaza kimya"Alisema kwa masikitiko makubwa.
Tarehe 25/4/ 2003 nikamuandikia barua waziri wa sheria na katiba wa wakati huo ili anisaidie kupata haki yangu lakini pia sikupata majibu na wala sikuchoka mpka tarehe 13/ 4/2006 nikaandika barua nyengine kwenda kwa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani sasa hapo kuna majibu yalitoka nafikiri walipewa maelekezo jeshi la polisi na walinijibu ".
Walinijibu hivi anasema mzee Massoud
" walinijibu kupitia hiyo barua kwa kuniambia kuwa sikuwahi kusimamishwa kazi nilifukuzwa kazi kwa fedheha ,wakati kosa mimi sikuenda kazini siku mbili bila taarifa na nilikuwa nasababu ambayo ni kuumwa na wasi wasi matatizo ambayo niliyapata vitani Uganda".
" Kitendo cha Fedheha ni kukamatwa na rushwa,kufanya ngono kazini
Kupigana na watu ukiwa na sare za kazi na makosa mengine makubwa na wala sio kutokwenda kazini siku 2 hilo ni kosa jengine".
kwa zaidi ya miaka 10 sasa amekuwa akifuatalia haki zake alizozikosa kutoka kwa jeshi hilo lakini ameshindwa kuzipata ,na batua hii ilitiwa saini na inspector jenerali wa jeshi la polisi Mashayo iliyotiwa saini kwa niaba ya inspector generali ."
Aidha Akieleza kuhusu barua nyengine aliyojibiwa 7/ 6/2006 mzee Massoud alieleza kuwa kufuatia kosa lake la kutokwenda kazini siku 2 alitiwa hatiani kwa kosa la utovu wa nidhamu huku akipewa adhabu ya kufukuzwa kazi kwa fedheha.
" Namlilia mama mtetezi wa wanyonge anisaidie jee hii ni haki ! na barua hii mwisho ilinitaka kama sijapata dischage yangu niende kwa kamanda wa polisi anisaidie "Alieleza
Nimeuza vipande vyangu vya ardhi kwajili ya kusomesha watoto wangu lakini hivyo bado nashindwa kuwaendeleza ,mama nisaidie wewe ndio mtetezi wa wanyonge ambae unapenda haki kwa wananchi wako uwezo wa kuwafikia siwi wananchi wa chini ni kupitia vyombo vya habari".
"Niliamini ipo siku nitaipata haki yangu kwa kuja kiongozi ambae atatusikiliza nilitamani hata nionane na Hayati Magufuli lakini ilishindikana hata mama Samia natamani nionane na wewe ana kwa ana lakini imeshindikana namuomba unisaidie kulifanyia uchunguzi hili ili niweze kupatiwa stahiki zangu utakapoziona habari hizi Alisema ".
" Nambari yangu ya kazi ni Z.1912 PC Masoud H.Omar Nimeshafuatilia vya kutosha kwa jeshi la polisi tangia nakwenda mwenyewe mpka naaandika barua lakini lakushangaza sijawahi kuitwa huko jeshi la polisi kupewa barua ya kuachishwa kazi, jengine ni kuambiwa nimefukuzwa kwa fedheha malalamiko haya leo nayapeleka kwa mama Samia yeye ndio mtetezi wetu sisi wananchi wanyonge.
"Ugonjwa ulionisababisha kutokuhudhuria kazini umetokana na mambo yale tuliyopitia tukiwa huko vitani Uganda mama Samia naamini kuapata haki zangu kupitia wewe na kwa sababu wewe ni mwenye huruma na ubinaadamu kwa watu wote "
Mwisho
Comments
Post a Comment