ZMBF YAFUNGA KAMBI SIKU 5 MICHEWENI KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA MBALI MBALI .
NA AMINA AHMED MO'HD.
Taasisi ya zanzibar maisha bora faundation imesema itaendelea kuunga mkono upatikanaji wa huduma bora za matibabu kwa wananchi visiwani zanzibar ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya nane katika uboreshwaji wa huduma za matibabu kwa wananchi wake.
Kauli ya mweneyekiti wa taasisi hiyo Maryam Mwinyi imetolewa kwa niaba na mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib Alipokuwa akizungumza na wananchi mbali mbali mara baada ya kumaliza bonanza maalum lililoanzia katika eneo la kilindini na kumalizika katika viwanja vya Shaame mata ikiwa ni uzinduzi wa kambi ya maisha bora afya bora iliyoandaliwa na taasisi hiyo .
Amewema licha ya taasisi hiyo kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbali mbali kwa wanachi 8000 upande wa kisiwani unguja lakini pia imelenga kutoa huduma ya uchunguzi kwa wagojwa 5000 kwa upande wa kisiwa cha Pemba kupitia kambi hiyo .
Amesema lengo la kambi hiyo nikuhakikisha wananachi wanaishi katika maisha bora huku wakiwa na afya njema.
Nae afisa Mtendaji mkuu wa tasisi hio Fatma Fungo amasema tasisi yao chini nya program ya maisha bora afya bora imeshatoa huduma ya matibabu kwa wannachi zaidi ya elfu Nane kupitia kambi mablimbali wanazoziweka ,huku kambi hio inatarajiwa kuhudumia zaidi ya Wananchi elfu 5.
Mapema Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Wemba Khamis Bilali amesema wizara ya Afya imejipanga kutoa huduma mbalimbali za Afya kwa Wananchi wote watakaokuja katika kambi hio.
Uzinguzi wa kambi hio ya siku 5 ambayo imeandaliwa na tasisi ya maisha bora foundation chini ya program ya maisha bora afya bora ilianzia na matembezi na mazoezi ya viungo
Comments
Post a Comment