WANANCHI CHAKE CHAKE WAASWA MASHIRIKIANO KUGUNDUA WAGONJWA WAPYA WA KIFUA KIKUU.

AMINA AHMED MOH'D.


WANANCHI wa wilaya ya Chake Chake  wametakiwa kutoa mashirikiano kwa  kwa wataalamu wa afya ambao wataendeleza zoezi la  kuwafuatilia  wagonjwa wapya wa kifua kikuu (TB)  ili lengo la kuinusuru jamii juu ya ugonjwa huo liweze kufikiwa .
     KHATIB JUMA MJAJA   -  DC MKOANI
Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya wa Chake Chake  Abdalla Rashid  Ali imetolewa   kwa niaba yake na  Mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja  alipokuwa akizungumza nao  katika mkutano wa ufunguzi    wa mradi  wa miezi 15 wa kuimarisha ufuatiliaji wa wagonjwa wapya  kifua kikuu  ( TB )  katika jamii (TBCI ) unaotekelezwa na jumuia ya wauguzi  "Zanzibar Nurses" Association   ( ZANA  )  huko katika  ukumbi wa maabara ya afya ya jamii ( PHL ) Wawi mapema leo.
               BAADHI YA WADAU 
Amesema lengo  la serikali kuruhusu jumuia  binafsi  kutekeleza  shughuli za kitaaluma  ni kuweza kusaidia kuona changamoto katika masuala tofauti ikiwemo masuala ya afya na kuweza kusaidiana nao  katika  kuleta mageuzi katika jamii hivyo mashirikiano hayo yatasaidia kuweza kuwagundua wagonjwa wapya na kupata matibabu kwa urahisi .

" Ugonjwa wa TB  bado ni changamoto  hususan ni kwa vijana   hivyo ni waase   wananchi  Chake chake na kusini yote  kutoa mashirikiano  katika kuona ugonjwa huu unadhibitiwa kwa kupatiwa tiba.

Aidha mkuu huyo ameipongeza jumuia ya wauguzi zana kwa mradi huo ambao unalengo la kuisaidia serikali katika kuimarisha  afya za wanachi wake .

"Serikali kuu haiwezi kutekeleza kila kitu ZANA  wameona changamoto  hii ya ugonjwa wa kifua kikuu TB  ambayo haipo wilaya ya Chake chake  tu takriban dunia nzima inaugonjwa huu tunashukuru kwa kuasisi mradi huu  ambao unakwenda kuwagusa wananchi moja kwa moja huku ikigusa  dhamira njema ya Rais wa Zanzibar  Dk Hussein Ali Mwinyi  katika kuimarisha huduma za matibabu nchini.

Hata hivyo  ametaka wanajumuia hiyo kuzidisha kutoa elimu  juu ya ugonjwa huo  wa ( TB ) kwa wanajamii ili waweze kuzijua dalili zake  na namna ya kijikinga.

Akizungumza  kuhusu utekelezaji wa mradi huo Msaidizi mratibu  wa mradi huo  wa kuwagundua wagonjwa wapya katika jamii  Mwajuma Ali Shehe amesema  utekelezaji wa mradi huo  uliofadhiliwa na  ( J S I  ) unatarajiwa kuibua wagonjwa 2720 katika wilaya hiyo ambao wanatarjiwa kufanyiwa  uchunguzi kupitia familia na jamaa wagonjwa  wa TB maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo ili kupatiwa tiba.
  MWAJUMA ALI  SHEHE   KAIMU AFISA MRADI.
Awali akizungumza  katibu wa Jumuia ya ZANA Pemba Othman Bakari Mohamed amesema  jumuia hiyo imekuwa msatari wa mbele katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kijamii ambayo inalengo la kuleta mabadiliko ya kiafya katika jamii .


 Shehia 10 ndani ya  wilaya ya Chake chake ambazo zinatarajiwa kunufaika na mradi huo  wa kuwagundua wagonjwa wapya wa Kifua kikuu  katika jamii  kwa awamu ya kwanza ambapo Utekelezaji wa mradi huo unatafanyika katika mikoa miwili  ya Zanzibar ikiwemo  mkoa wa mjini maghrib pamoja na mkoa wa Kusini Pemba  huku Shehia nyengine kumi  kwa upande wa wilaya ya Mkoani zikitarajiwa kunufaika na mradi huo    .

Aidha mada juu ya kifua kikuu pamoja na kifua kikuu sugu ni miongoni mwa mada zilizofundishwa kwa wadau hao  wakiwemo viongozi wa shehia ,viongozi wa dini,wauguzi,wasimamizi wa vituo vya afya vya serikali na binafsi watu wenye ulemavu  ndani ya wilaya hiyo wameshiriki katika mkutano huo huku mkutano kama huo kwa  wadau kutoka wilaya ya Mkoani ukitarajiwa kufanyika  kesho.
 

Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.