WAMILIKI VYOMBO VYA MTANDAO PEMBA WAASWA HAYA

Na Amina Ahmed Moh'd

AFISA  Mdhamini Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau  amewataka waandishi wa Habari  kufanya kazi kwa kuzingatia  maadili na sheria za uwandishi wa Habari.
Aliyasema hayo  wakati alipokua akizungumza na waandishi wa Habari Pamoja na wamiliki wa vyombo vya Habari vya mitandao huko ukumbi wa zbc mkoroshoni  ,Wilaya ya chake chake mkoa wa kusini Pemba.

Mfamau alisema mwandishi wa Habari bora ni yule anaezitangatia misingi na maadili ya kazi yake ,huku akiepukana na Habari zilisoleta tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Mdhamin huyo alisema kalamu ya mwandishi inaweza kujenga amani ama kubomoa amani iliyopo ,hivyo ni wajibu wa mwanadishi wa Habari kuitumia kalamu yake vyema katika kuandika Habari zake.

“Jambo la kusikitisha kuna watu wanaivamia hii ,huku wakiwa hawajui misingi na maadili ya uwandishi wa Habari na kupelekea kuandika Habari za uongo na zisizo na madili”Alifafanua.

Aidha Mfamau alisema Seikali ya Mapinduzi Zanzibar  imetengeneza mazingira mazuri ya kila tasnia  ,hivyo niwajibu wetu kufata taratibu na kupata fanim hizo.

Pamoja na hayo amewataka wamiliki wa vyombo vya Habari kuhakikisha wanafuata sheria za tume ya utangazaji  huku wakiwakatia leseni ya uwandishi wa Habari Wanadishi wao.

“Hili ya leseni ya uwandishi wa Habari ni lazima kwa kila mwandishi wa wahabari kuwa nayo ,lesini hio ndio itakayotusaidia kuwakatama wale waqnayoingilia fani hio “Alisema Mfamau.

Mdhamini Mfamau alisema hatomfumbia macho mtu yoyote mwenye lengo la kuichafua fani hio na yule mwenye kwenda kinyume na maadili ya sheria .

Kwa upande wake Katibu mtendaji Tume ya utangazaji Zanzibar   Suleiman Abdulla Salim aliwataka waandishi wa Habari kuandika Habari  za ukweli  na za usawa kwa pande zote.
Pia aliwatataka wamiliki wa vyombo vya Habari kuhakikisha vyombo vyao vimesajiliwa katika Tume ya Utangazaji ili kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza.

                                                 MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

UHABA WA VITUO VYA POLISI WILAYA YA CHAKE CHAKE BADO MLIMA MREFU KUDHIBITI UHALIFU VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAMU.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.