VIJANA MKOANI WALIA KUTOSHIRIKISHWA KATIKA MASUALA YA UCHAGUZI
Na Amina Masoud.
VIJANA Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba wamesema licha ya kutokuwa na elimu ya uongozi lakini pia kuna kikwazo cha kutoshirikishwa juu ya masuala hayo.
Wakizungumza katika mjadala wa wazi uliofanyika katika viwanja vya skuli ya michenzani msingi kijana Faida Makame Shaali na Faki Sharif Nahoda wamesema bado elimu ya uongozi ni ndogo kwao lakini pia kunachangamoto baadhi ya viongozi kutowashirkisha juu ya mambo yanayowahusu jambo ambalo linapelekea kuwa nyuma kushiriki katika harakati za uongozi.
Wameeleza kuwa endapo kutatolewa fursa na ushirikishwaji wa vijana katika uongozi inaweza kusaidia vijana walio wengi kushiriki katika harakati hizo.
Kwa upande wake diwani kijana Mohd Said Ali amesema licha ya changamoto hizo lakini bado kama vijana wanayofursa ya kutafuta namna ya kushiriki katika uongozi kwani vijana ni ndio tegemeo la taifa.
Afisa vijana wilaya Mkoani Stara Khamis Salum amewataka vijana hao kutokuvunjika moyo kwani serikali imeegeza nguvu zake Zaidi kwa vijana hivyo ni vyema kuchangamkia fursa zilizopo.
Sambamba na hayo amesema sera ya maendeeo ya vijana ya mwaka 2023 dhamia yakeni kukuza ustawi wa maendeleo ya vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi na endelevu yatakayoimarisha ushiriki na ushirikishwaji wao katika Nyanja za kiuchumi,kijamii na kisiasa.
Kwa upande wao wazazi walioshiriki katika mjadala huo wameiomba serikali kutoa elimu kwa vijana kuhusu masuala ya uongozi ili iwe rahisi kuingia katika harakati hizo.
Mdajadala huo wa wazi ulioandaliwa na radio jamii mkoani ukiwa na lengo la kuangalia ni changaoto gani zinawakwaza vijana kuingia katika harakati za uongozi umefanyika katika viwanja vya skuli ya michenzani wilaaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba na kushirikisha vijana wazazi Pamoja viongozi wa serikali.
MWISHO.
Comments
Post a Comment